Aliyekuwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tawi la Isitu, Chimara mkoani Mbeya, Felix Komba jana alizolewa na Operesheni ya M4C Pamoja Daima ya Chadema na kuamua kukikacha chama chake na kujiunga na chama hicho.

Operesheni hiyo ya Chadema inayozunguka nchi nzima imeendelea kushika kasi kutokana na maelfu ya wananchi kujitokeza katika mikutano ya chama hicho.

Operesheni hiyo imezidi kuwa tishio kwa CCM kutokana na kuongezeka kwa mashabiki wa chama hicho kwa kipindi hichi. Zifuatazo ni picha za mikutano ya M4C Pamoja Daima iliyofanyika maeneo tofauti tofauti.


Click image for larger version. 

Name: 1.jpg 
Views: 50 
Size: 92.7 KB 
ID: 136
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe akihutubia wananchi wa mjini Ngara katika mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika jana.

Click image for larger version. 

Name: 2.jpg 
Views: 54 
Size: 90.5 KB 
ID: 137
Aliyekuwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tawi la Isitu, Chimara mkoani Mbeya, Felix Komba akizungumza katika mkutano wa Operesehni M4C Pamoja Daima mbele ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, baada ya katibu huyo kujiunga na Chadema wakati wa mkutano huo uliofanyika Chimara jana.

Click image for larger version. 

Name: 3.jpg 
Views: 46 
Size: 100.1 KB 
ID: 138
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa akiwahutubia wananchi wa mji wa Makambako, katika mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika jana.

Click image for larger version. 

Name: 4.jpg 
Views: 68 
Size: 101.5 KB 
ID: 139
Wananchi wa mji wa Njombe na vitongoji wakiwa katika mkutano wa hadhara wa Operesehni M4C Pamoja Daima, wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), uliofanyika mjini Njombe jana.

Click image for larger version. 

Name: 5.jpg 
Views: 43 
Size: 100.9 KB 
ID: 140
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi 'Sugu', akihutubia mkutano wa hadhara ikiwa ni mfululizo wa mikutano ya Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika katika mji wa Chamara mkoani Mbeya jana.