
Wakristo wa madhehebu ya Koptik nchini Misri wanapiga kura leo kumchagua
kiongozi mpya atakayechukua nafasi ya Baba Mtakatifu Shenuda wa tatu,
aliyefariki mwezi Machi mwaka huu.
Kifo cha Shenuda ambaye aliliongoza kanisa hilo kwa miongo minne,
kilianzisha mjadala wa kumchagua kiongozi mpya kuongoza jamii hiyo
katika utawala wa baada ya mapinduzi nchini Misri, ambao unakumbwa na
ongezeko la hofu ya kimadhehebu. Bruce Amani na mengi zaidiWagombea watano, ikiwa ni pamoja na maaskofu wawili na watawa watatu wanaume, wanawania nafasi ya kuwa Baba Mtakatifu wa 118 wa kanisa hilo barani Afrika. Baraza la viongozi wakuu, maafisa wa umma wa saa na wa zamani katika kanisa hilo, wabunge, madiwani na waandishi habari watapiga kura ya kuchagua mgombea wanayemtaka. Majina ya wagombea watatu watakaopigiwa kura nyingi kisha yataandikwa kwenye vijikaratasi tofauti na kuwekwa kwenye sanduku litakalokuwa juu ya madhabahu ya kanisa la mtakatifu Marko mjini Cairo.

Vuingozi hao wamekuwa wakizuru makanisa mbalimbali kote nchini humo kabla ya uchaguzi huo. Waumini wa kanisa la Koptik kote ulimwenguni waliombwa kufunga na kuomba kwa siku tatu kabla ya kupiga kura, na kipindi cha pili cha mfungo kitaanza mnamo oktoba 31.
Kiongozi mmoja ambaye hayuko kwenye orodha hiyo ni Askofu Bishoy aliye na msimamo mkali, kwa sababu ya mashambulzii yake ya dhidi ya madhehebu mengine, katika matamshi yake ya nyuma katika vyombo vya habari ambayo yangeweza kuzusha msuguano wa kimadhehebu nchini humo.

Kuongezeka maukundi ya wanamgambo wa kiislamu wenye itikadi kali, na kuchaguliwa kwa rais wa kwanza Muislamu Mohamed Morsi kumezusha hofu ya kutokea unyanyasaji wa wakristo wa Koptik licha ya ahadi za kila mara za Morsi kuwa atakuwa rais wa Wamisri wote.
Katika tukio la hivi karibuni, wakristo watano wa madhehebu ya Koptik walijeruhiwa jana Jumapili baada ya makabiliano kuzuka katika kanisa la kijiji kimoja kusini mwa mji mkuu Cairo.
Ghasia hizo zilizuka wakati wanakijiji Waislamu walipojaribu kufunga barabara inayoelekea katika kanisa hilo wakati waumini wa Koptik wakiwasili kanisani humo kuhudhuria ibada ya Jumapili. Utulivu ulirejea katika eneo hilo baada ya polisi kuingilia kati.
0 Maoni:
Post a Comment