Chondechonde Kikwete achana na agenda hiyo ya UPOLE, inakiua chama chako na serikali yako,

Ni karibu miezi 28 sasa, Edward Lowassa amekuwa agenda kuu ndani ya CCM na wanaccm wenye, si mwenyekiti wala mjumbe wote mioyo yao ni Lowasa tu, wengi wakitaka ajipambanue nakuwa nyota huru ya chama na wachache walio juu ya chama wakitaka kumpoteza gwiji huyu wa siasa za ukwasi na fitina msonge!

Ikumbukwe kuwa doa kuu linalotajwa kuwa Lowa ni fisadi ni Richmond, lakini nani asiyejua richmond ni nani na ilikuwaje? Pale dodoma Lowasa ameweka wazi mbele ya Mwenyekiti kuwa hakuna kilichotendeka ambacho mwenyekiti hakukijua ama kumtuma! Narudia tena UCHAFU wa LOWASSA ni RICHMOND tu!

Nauliza tena RICHMOND ni nani? Mwenyekiti alijibu nini siku ile pale Dodoma wakati lowassa anamhiji zaidi ya kuinamisha kichwa chini hali iliyopelekea BWM kumtuliza Lowasa?

Sasa Lowassa anakitaka Chama na agombee urais na ameshashinda ndani ya Chama na nusu uwanja nje ya chama, shime ccm, ili muendelee kuitwa chama cha siasa japo mwaweza kuwa wapinzani zuieni jaribio la mwenyekiti wenu la kujaribu kumzika Lowassa angali amekibeba chama!

Kuna juhudi za kitoto ndani ya ccm eti wapo kwenye harakati za kumuuandaa January Makamba kugombea Urais 2015, wanatumia raslimali za nchi kujijenga kisiasa kwa upinde wa mvua ya siasa!

Chondechonde mwenyekiti wa ccm ndugu Jakaya Mrisho Kikwete, Amini Lowassa ndie chaguo la wanaccm wote hata hao wanaojifanya wapo na wewe mioyo yao ipo kwa Lowassa! Wanakula na kunywa kwa mgongo wa Lowassa!

Mwenye USHAHIDI wa wazi juu ya UFISADI wa Lowassa aulete hapa, sio stori za kulishwa vijiweni kisha mnakuja hapa kupiga ngonjera ooho Lowasa fisadi, oooho sijui nini! Leteni utetezi hapa

Mimi nitampa kura yangu ikiwa atagombe japo hata shinda, lakini atakinusuru chama kufutika kabisa duniani!

Na: Yericko Nyerere