Thursday, February 7, 2013

Utulivu Tunisia baada ya mauaji



 
Inaarifgiwa polisi mmoja aliuawa kwenye maandamano hayo
Kumekuwa na utulivu mjini Tunis, Tunisia usiku kucha baada ya siku moja ya vurugu kufuatia mauaji ya mwanasiasa mashuhuri wa upinzani Shokri Belaid.
Waziri Mkuu wa Tunisia, Hamadi Jebali, amesema ataunda Serikali ya watalamu kufuatia mauaji ya Belaid.
Maelfi ya waandamanaji waitaka serikali tawala kujiuzulu kuhusiana na mauaji hayo.
Lakini mmoja wa viongozi wa serikali alilaani mauaji hayo akiyataja kuwa kitendo cha uoga na kuwa wale waliomuua kiongozi huyo hawatafanikiwa kusababisha vurugu Tunisia.
Mauaji ya Bwana Belaidi, ambaye amekuwa mkosoaji mkuu wa Serikali yalisababaisha ghasia katika miji kadhaa nchini. Waandishi wa habari kutoka eneo hilo wanasema kufikia sasa afisaa mmoja wa polisi ameuliwa na waandamanaji hao.
Jamaa za marafiki za marehemu Shokri Belaid
Akihutubia taifa katika matangazo ya moja kwa moja katika runinga Bwana Jebali alisema kuwa Serikali hiyo itaendelea kwa muda bila mwelekeo wa vyama hadi Uchaguzi Mkuu utakapofanywa.
Maelfu ya waandamanaji walikuwa wametoa wito kujiuzulu kwa chama kinachotawala cha Kiislamu cha ENNAHDA kufuatia mauaji ya Belaid.
Muungano wa vyama vya kiraia uliokuwa mwanachama wa serikali ya muungano, uliondoka Serikalini na kuitisha mgomo wa taifa lote.

0 Maoni:

Post a Comment