Tuesday, May 22, 2012

MBOWE,DK SLAA kulitikisa jiji la dar jumamosi hii


Viongozi wakuu wa CDM wakiongozwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dr Wilbroad Slaa Jumamosi ijayo tarehe 26/05/2012 watalitikisa jiji kuu la Dar kwa kufanya mkutano mkubwa wa hadhara katika viwanja vya Jangwani.

Mkutano huo utakuwa ni maalum kuzungumza na kuwaelimisha wananchi kuhusiana na Katiba mpya. Pia viongozi hao wanatarajiwa kulaani uamuzi wa halmashauri kuu ya CCM kutenga mambo kadhaa na kuwaamuru wananchi kutoyajadili kwani yanapaswa kubaki kwenye katiba kama yalivyo.

Mkutano huo pia utahudhuriwa na Naibu katibu mkuu Zitto Kabwe, Mnadhimu mkuu wa upinzani Tundu Lissu, Mwanasheria maarufu Mabere Marando,wabunge wote wa chama hicho na wajumbe wote wa kamati kuu.

Itakumbukwa mara ya mwisho CDM kufanya mkutano mkubwa kama huo Dar ni siku ya uzinduzi wa kampeni za mgombea urais wa chama hicho mwezi Agosti mwaka juzi.

Mkutano huo unatarajiwa kulitikisa jiji la Dar na Taifa kwa ujumla kwani Maelfu ya wana-CCM wanatarajiwa kuvua Gamba na kuvaa Gwanda.

Source: John Mnyika-CDM

0 Maoni:

Post a Comment