Hali ya kaskazini mwa Mali ni ya hatari, kiasi kwamba, bila ya msaada wa
jumuiya ya kimataifa haiwezi kudhibitika tena.Na uwezekano wa nchi za
Afrika magharibi kujiingiza kijeshi katika nchi hiyo unazidi kuwa mkubwa
Kansela wa Ujerumani pia amesema Ujerumani ipo tayari kutoa mafunzo ya
kijeshi ili kusaidia nchini Mali. Hali ya kaskazini mwa Mali imeshaenda
mrama. Makundi ya waislamu wenye itikadi kali , yenye uhusiano na
al-Qaeda yanawanyanyasa watu. Sehemu hiyo haina polisi tena.Na kwa
mujibu wa taarifa wapiganaji wa jihad kutoka nje wanamiminika katika
sehemu hiyo.
Watu sasa wanaanza kuiita Mali kuwa ni Afrighanistan-yaani Afghanistan
ya barani Afrika kwani uwezekano wa jumuiya ya kimataifa kujiingiza Mali
kijeshi unazidi kuwa mkubwa. Ujerumani pia imesema ipo tayari kutoa
mafunzo ya kijeshi ili kuisaidia serikali ya Mali katika harakati zake
za kupambana na makundi ya watu wenye siasa kali kaskazini mwa nchi
hiyo.
Watu katika sehemu hiyo wanaishi katika hali mbaya . Mama mmoja amesema
watu wanabakwa, wanapigwa na wanauliwa.Amesema wanaishi katika madhila
makubwa. Iwe ni katika mji wa Timbuktu, Gao au Kidal inapepea bendera
nyeusi ya waislamu wenye itikadi kali. Watu walioshamiri kwa silaha,
wenye vilemba na ndevu ndefu, wanavinjari barabarani katika magari yao.
Polisi wao ndiyo wanaotoa mwongozo wa maisha, kwa mujibu wa sheria ya
kiislamu.
Sehemu ya kaskazini mwa Mali inadhibitiwa na watawala wapya -yaani
Waislamu wenye itikadi kali, kama vile Ansar dine au Wanajihadi wa
Mujao,Shule nyingi zimefungwa,watoto wanaandikishwa jeshini kwa nguvu,
na wanawake wasiofunika nyuso zao wanakuwa katika hatari ya kutiwa ndani
au mambo yanaweza kuwa mabaya zaidi kwao.
Maafa makubwa yanatokea kaskazini mwa Mali .Watu wanatandikwa viboko
kila siku,wanapigwa mawe na wanakatwa sehemu za miili yao.Pamoja na hayo
yote Waislamu wenye itikadi kali wanaziteketeza turathi za utamaduni wa
dunia.
Lakini jumuiya ya kimataifa sasa haitaki kuendelea kusubiri. Baraza la
Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa ridhaa ya kuchukua hatua za kijeshi
kaskazini mwa Mali. Umoja wa Afrika na Jumuiya ya uchumi ya nchi za
Afrika magharibi pia zinatayarisha mpango wa kuikomboa Mali ya kaskazini
kwa kutumia nguvu za kijeshi. Kamishna wa masuala ya amani na usalama
kwenye Umoja wa Afrika Ramtane Lamamra ameeleza kwamba sasa pana
mabadiliko katika msimamo wa jumuiya ya kimataifa kuhusu mgogoro wa
nchini Mali.Amesema kwa kusimama pamoja mgogoro huo utatatuliwa kwa
mafanikio.
Lakini jambo moja ni wazi kabisa, kwamba serikali ya Mali haitaweza kuutatua mgogoro wa kaskazini mwa nchi hiyo peke yake
0 Maoni:
Post a Comment