Mkutano muhimu wa kilele kuhusu mustakbal wa Umoja wa Ulaya unalenga
kuweka kando masilahi ya kitaifa,na kuafikiana kuhusu bajeti ya
kugharimia miradi ya kubuni nafasi zaidi za kazi hadi ifikapo mwaka 2020
"Ulaya yenye nguvu bila ya kulazimika kutoa pesa zaidi":huo ndio msimamo
ambao Ujerumani inatapanga kuutetea katika mazungumzo ya kubuni bajeti
ya muda mrefu ya Umoja wa Ulaya.Pale viongozi wa taifa na serikali wa
mataifa 27 watakapokutana kuanzia leo alkhamisi hadi kesho ijumaa mjini
Brussels,serikali kuu ya Ujerumani inataka kuona gharama zote za Umoja
wa Ulaya katika kipindi cha mwaka 2014 hadi 2020 zinaambatana ipasavyo
na mahitaji halisi.Matumizi bora ndio kauli mbiu ambayo kwa kansela
Angela Merkel haimaanishi chengine isipokuwa kupunguzwa bajeti ya Ulaya
ya mabilioni ya Euro.
Ujerumani inachangia moja kwa tano ya bajeti jumla ya Umoja wa Ulaya
kiwango ambacho kinafikia Euro bilioni 200 ikizingatiwa bajeti ya
kuanzia mwaka 2007 hadi mwaka huu wa 2013.Wakati wa mkutano pamoja na
waziri mkuu wa Italy Mario Monti hapo awali mjini Berlin,kansela Angela
Merkel alikumbusha kwamba"Ujerumani ni mojawapo ya wachangiaji wakubwa
miongoni mwa nchi za Umoja wa Ulaya,Na hiyo ndio maana wanapendelea
kuona kwamba fedha zinatumiwa kwa namna ambayo zitachangia ipasavyo
kuufanya Umoja wa Ulaya uzidishe bidii na kuwa uwanja muhimu wa
mashindano ya kibiashara."
Upinzani wa nchi za kusini mwa ulaya
Hata alipokutana na waziri mkuu wa Hispania Mariano Rajoy na rais
Francois Hollande wa Ufaransa,hakuchelea kansela kutilia mkazo madai ya
Ujerumani,siku chache kabla ya mkutano huo wa kilele kuanza.
Sambamba na kupunguza nakisi,kanasela Angela Merkel anataka pia matumizi
katika bajeti ya pamoja ya Umoja wa Ulaya yawekewe kikomo.
"Matumizi ya Umoja wa Ulaya yanabidi yasiruhusiwe kupindukia asili mia
moja ya pato la kijamii katika Umoja wa Ulaya-amesema mchambuzi wa
masuala ya fedha wa Umoja wa Ulaya Friedrich Heinemann wa taasisi ya
uchunguzi wa kiuchumi ya mjini Mannheim.Inamaanisha kwamba bajeti ya
Umoja wa Ulaya iongezeke tu ikiwa shughuli za kiuchumi za nchi za Umoja
huo zitanawiri na kwa namna hiyo kuongezeka pia pato la ndani la kila
mkaazi wa Umoja wa ulaya.
Nchi nyingi za Umoja wa Ulaya,ikiwa ni pamoja na
Austria,Finland,Itali,Uholanzi na Sweden zinauunga msimamo wa
Ujerumani.Lakini nchi zinazopokea misaada mfano wa
Uhispania,Ureno,Ugiriki na nyengine zinaupinga.
Ajira ya vijana ndio kipa umbele
Ujerumani inataka kuona fedha nyingi zaidi zikitolewa kugharimia miundo
mbinu ya nishati na miradi ya uchunguzi barani Ulaya.Halmashauri kuu ya
Umoja wa Ulaya inapendekeza Euro bilioni 120 kwaajili ya miradi
hiyo.Katika bajeti ya mwaka 2007 hadi mwaka huu wa 2017 asili mia 80 ya
bajeti ya Umoja wa Ulaya ilikuwa ikitumika kusaidia shughuli za kilimo
na miradi mengine ya kimkoa.Ujerumani ingependelea kuona fedha za
kughamiria miradi ya kilimo na kimkoa zinafutwa.Katika wakati ambapo
Ufaransa inataka kuona fedha hizo zinaendelea kutolewa Ujerumani inataka
kuona zinatumika kupambana na ukosefu kazi miongoni mwa vijana.
0 Maoni:
Post a Comment