Sunday, January 20, 2013

Nchi zaidi ya 140 zimekubaliana kuchukua hatua za kuzuwia matumizi ya zebaki ambayo inachafua mazingira.



Thermometer yenye mercury
Wajumbe katika mkutano wa Umoja wa Mataifa mjini Geneva walikubaliana kupunguza, na hatimaye kumaliza kabisa, utumizi wa madini hayo yenye sumu ambayo inatumiwa kwenye zana kadha za majumbani kama zana za kupimia joto, yaani thermometers.
Piya walikubaliana kupunguza zebaki inayotoka kwenye vinu vya nishati na karakana za kutengeneza saruji.
Wachimba migodi wadogo-wadogo wanaotumia zebaki kutenganisha dhahabu na udongo wanafaa kupewa hifadhi.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira, UNEP, limesema mkabata huo unaweza kuchukua hadi miaka mitano kuanza kutekelezwa.


Chanzo: BBC

0 Maoni:

Post a Comment