Saturday, January 19, 2013

Dr. Slaa na makamanda wengine kutikisa msimbazi centre kongamano la wanavyuo.


KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, leo anatarajiwa kufungua kongamano la wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyoko Dar es Salaam.



Akizungumza na gazeti hili, Mwenyekiti wa Muungano wa Wanafunzi wa CHADEMA Vyuo Vikuu (CHASO) mkoani Dar es Salaam, Freddy Chacha alisema kongamano hilo litafanyika katika Ukumbi wa Msimbazi Center. Alisema katika kongamano hilo, vijana wanatarajiwa kuwaapisha viongozi wa shirikisho hilo kwa 

Mkoa wa Dar es Salaam, kueleza mipango mipya kuelekea mwaka 2015, kutambulisha matawi na viongozi wake kwa viongozi wa kitaifa. Pia kuandikisha wanachama wapya na kutoa tamko lao dhidi ya vijana waliofanya usaliti, na kuanza kuichafua Chaso kwa kueneza harakati mbaya za CCM dhidi ya CHADEMA.

Mwenyekiti huyo alisema pamoja na Dk. Slaa, viongozi wengine wa chama hicho wanaotarajiwa kuwepo ni Mbunge wa Ubungo, John Mnyika; Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema; Mwenyekiti wa BAVICHAf Taifa, John Heche; Mhadhiri wa Chuo Kikuu na Mkuu wa Kitivo cha Elimu katika Chuo Kikuu kishiriki cha Chang’ombe, Dk. Kitila Mkumbo. 

Mwenyekiti huyo alivitaja vyuo vitakavyoshiriki kuwa ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Taasisi ya Utawala wa Fedha (IFM), Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU), Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Chuo Kikuu cha Kampala (KIU),Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Teknolojia yaMadawa (IMTU), Chuo cha Ustawi wa Jamii,Chuo Kikuu cha Mtakatifu Yohane na Chuo Kikuu cha Muhimbili.

0 Maoni:

Post a Comment