Sunday, January 20, 2013

DCI Manumba akata kauli

na Lucy Valentine na Andrew Chale AFYA ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai wa Jeshi la Polisi nchini (DCI), Robert Manumba inazidi kuwa mbaya baada ya kuwapo taarifa kwamba amekata kauli na mawasiliano kwa siku tatu mfululizo, huku akiendelea kupumua kwa msaada wa mashine. Hali hiyo tete ya afya yake imesababisha kuwapo kwa usiri mkubwa kutoka kwa maofisa wa Jeshi la Polisi, madaktari wanaomtibu na ndugu zake. Akizungumza na waandishi wa habari kwa kifupi sana, Daktari Mkuu wa Hospitali ya Aga Khan alikolazwa, Jaffer Dharsee alisema kuwa atakuwa tayari kueleza maendeleo ya matibabu ya Manumba Jumatatu ijayo. “DCI Manumba bado yupo katika chumba maalumu akiendelea na matibabu chini ya uangalizi maalum wa madaktari na wauguzi,” alisema Dk. Dharsee. Hata hivyo, uchunguzi uliofanywa na gazeti hili katika viwanja vya hospitali hiyo jijini Dar es Salaam, umebaini kuwa hali ya DCI huyo inakatisha tamaa. Hali hiyo ndiyo imeifanya serikali kushindwa kumsafirisha nje ya nchi kwa matibabu zaidi. Hakuna mtu anayeruhusiwa kuingia kumwona isipokuwa kwa baadhi ya viongozi na ndugu wachache muhimu. Manumba aliugua ghafla na kulazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, akipatiwa matibabu kwa kile kilichoelezwa kuwa na wadudu wengi wa ugonjwa wa malaria. Hata hivyo, Januari 14, alihamishiwa katika Hospitali ya Aga Khan kwa matibabu zaidi na kuwekwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi. Manumba aliteuliwa na Rais Kikwete kushika wadhifa huo mwaka 2006, akichukua nafasi ya Adadi Rajabu

0 Maoni:

Post a Comment