Kampeni za uchaguzi wa ugombea udiwani zimezidi kuwasha moto wakati tukielekea siku ya uchaguzi ambayo ni tarehe 28/10/2012 siku ya Jumapili.Halikadhalika kampeni hizo zimeendelea mkoani Shinyanga hususani kata ya Mwawaza ambayo ushindani mkubwa upo kati ya CCM na CDM.

Leo kwenye viunga vya uwanja wa shule ya msingi Ugimbagu,mh.Vicent Josephat Nyerere amewatahadharisha wananchi wa kata hiyo kuwa makini wanapofanya maamuzi mazito juu ya mstakabali wa maisha yao kwa kutumia haki yao ya kikatiba ya kumchagua kiongozi atayeweza kutekeleza shida na matakwa ya wana Mwawaza.

Huku akimnadi mgombea wa chama chake cha CDM,mh Vicent amewashangaa wananchi ambao miaka zaidi ya hamsini hawana huduma muhimu za kijamii kama vile maji,umeme na huduma za afya lakini wanathubutu kuing'ang'ania CCM,wakati CCM ina wenyewe.

Imekuwa ni desturi kwa CCM kuwakumbuka wananchi wa kata hiyo kila inapofika kipindi cha uchaguzi huku ikinadi ahadi mpya kabisa na kusahau kuwa wameshindwa kutekeleza ahadi walizo ahidi huku siku za nyuma.Akiwasihi wananchi hao ambao kwao huduma ya maji inaonekana kama anasa alisema CM ya leo si CCM ya mwalimu J K Nyerere,CCM ya mwalimu iliwajali wananchi na ilikuwa kweli CCM ya wakulima na wafanyakazi lakini leo hii CCM imekuwa kichaka cha wahalifu mbalimbali ambao wanatumia pesa chafu kuhakikisha wanapita katika chaguzi mbalimbali ili waweze kusimamia maslahi yao binafsi.

Uchaguzi wa ndani ya CCM umethibitsha kuwa mlalahoi hana nafasi ndani ya chama tofauti na CCM ya mwalimu.CCM ya mwalimu ni sawa na CDM ya leo ambayo inawajali wananchi wake na kuwapigani kwa hali na mali kufanikisha maisha yao na rasilimali zao zinasimamiwa kwa manufaa ya umma.

Akibeza tabia iliyojitokeza leo ndani ya chama tawala,ameshangazwa na kauli ya M/Kiti kukiri utitiri wa rushwa ndani ya chaguzi za chama huku akishindwa kuzifuta chaguzi zote ambazo zimekichafua chama.

Akilaani matukio ya uvunjivu wa amani ndani ya kata hiyo, yeye kama waziri kivuli wa mambo ya ndani amemtaka waziri wa mambo ya ndani kuhakikisha watu wote waliofanya tukio la kushambulia M/kiti wa tawi la Mwawaza kwa kumchoma mkuki kukamatwa mara moja ikiwa na kuwatia nguvuni wale wote walio washawishi vijana hao kufanya ukatili kama huo vinginevyo ajiuzuru nafasi yake ya uwaziri wa mambo ya ndani.

Tukio hilo la kushambuliwa M/Kiti huyo limeibua simanzi kubwa miongoni mwa wananchi wa kata hiyo na kukosa kabisa imani na serikali ya CCM. Nikiongea na mmoja wa wakazi wa maeneo ya Ugimbagu, mwananchi huyo amelaani kitendo alichofanyiwa kiongozi wao na kusema, matokeo ya serikali kuwatelekeza wananchi kwa zaidi ya miaka hamsini malipo yake ni kuwapiga mishale na risasi za moto.