Friday, October 19, 2012

Askofu Malasusa: Tumechoka na ghasia Ijumaa, Octoba 19, 2012 05:25 Na Christina Gauluhanga, Dar es Salaam KANISA la Kiinjili la Kiluteri Tanzania (KKKT), limesema limechoshwa na vitendo vya hujuma wanavyofanyiwa Wakristo vinavyoashiria vita na kuiomba Serikali kufanya kila njia kulinusuru taifa. Kauli hiyo, ilitolewa jana mjini Dar es Salaam na Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Dk. Alex Malasusa. Alisema vitendo vinavyofanywa na Waislamu kama havitaangaliwa kwa undani, vinaweza kuchochea mauaji ya watu na kupoteza amani iliyopo. Alisema uvumilivu walionao Wakristo, si ujinga wala woga, bali ni busara tu. "Ni busara tu Wakristo kuamua kunyamazia mambo haya, lakini naomba isiwe ni fimbo ya kutuachia kila kukicha tunanyanyaswa na kundi hili dogo la watu wenye nia mbaya na nchi," alisema Malasusa. Alisema ukimya wa vyombo vya dola juu ya vitendo vya uvunjaji wa sheria, hauna maslahi kwa taifa na kufananisha vitendo hivyo sawa na mauaji ya kimbari. Alisema kwa muda mrefu, kundi hilo limekuwa likiachiwa, kitendo kinachofanya liendelee kutamba mitaani. “Kila kukicha wanaendelea kulitia hasara taifa kwa kusababisha uchochezi wa kidini na kuwafanya wananchi kuwa na hofu wakati wote. "Tunakumbuka hawa ndugu zetu, walivyovamia pale wizarani na kushinikiza wenzao waachiwe, katika mazingira ya kutatanisha waliachiwa na hakuna waliochukuliwa hatua… hiki maana yake nini?” alihoji Askofu Malasusa. Alisema endapo jitihada za makusudi za kuzuia hali hii hazitachukuliwa, kila kukicha tutayasikia makubwa zaidi, huku vituo vya polisi na Mahakama zikiendelea kudhalilishwa kwa kuchomwa moto na kuamsha hasira kwa askari kurusha mabomu na risasi za moto. "Hivi katika hili Serikali inasubiri kundi hili lifanye nini ili iamke usingizini na kuvidhibiti vitendo vinavyofanywa na watu hao wanaojiita wanaharakati wa kutetea dini ya Uislamu na ndiyo maana kila kukicha tunaona hali ya kutishia amani ya nchi, misikiti ikitekwa, uhai wa viongozi wa dini ukitishiwa hadharani, viongozi wastaafu wakizabwa vibao hadharani kwa sababu za harakati za kidini," alisema. Akitoa msimamo wa kanisa hilo, Mkuu wa Dayosisi ya Ushirika wa Meru, Askofu Paulo Akyo, alisema kilichotokea Mbagala katika wiki .

Askofu Malasusa: Tumechoka na ghasia

KANISA la Kiinjili la Kiluteri Tanzania (KKKT), limesema limechoshwa na vitendo vya hujuma wanavyofanyiwa Wakristo vinavyoashiria vita na kuiomba Serikali kufanya kila njia kulinusuru taifa.

Kauli hiyo, ilitolewa jana mjini Dar es Salaam na Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Dk. Alex Malasusa.

Alisema vitendo vinavyofanywa na Waislamu kama havitaangaliwa kwa undani, vinaweza kuchochea mauaji ya watu na kupoteza amani iliyopo.

Alisema uvumilivu walionao Wakristo, si ujinga wala woga, bali ni busara tu.

"Ni busara tu Wakristo kuamua kunyamazia mambo haya, lakini naomba isiwe ni fimbo ya kutuachia kila kukicha tunanyanyaswa na kundi hili dogo la watu wenye nia mbaya na nchi," alisema Malasusa.

Alisema ukimya wa vyombo vya dola juu ya vitendo vya uvunjaji wa sheria, hauna maslahi kwa taifa na kufananisha vitendo hivyo sawa na mauaji ya kimbari.

Alisema kwa muda mrefu, kundi hilo limekuwa likiachiwa, kitendo kinachofanya liendelee kutamba mitaani.

“Kila kukicha wanaendelea kulitia hasara taifa kwa kusababisha uchochezi wa kidini na kuwafanya wananchi kuwa na hofu wakati wote.

"Tunakumbuka hawa ndugu zetu, walivyovamia pale wizarani na kushinikiza wenzao waachiwe, katika mazingira ya kutatanisha waliachiwa na hakuna waliochukuliwa hatua… hiki maana yake nini?” alihoji Askofu Malasusa.

Alisema endapo jitihada za makusudi za kuzuia hali hii hazitachukuliwa, kila kukicha tutayasikia makubwa zaidi, huku vituo vya polisi na Mahakama zikiendelea kudhalilishwa kwa kuchomwa moto na kuamsha hasira kwa askari kurusha mabomu na risasi za moto.

"Hivi katika hili Serikali inasubiri kundi hili lifanye nini ili iamke usingizini na kuvidhibiti vitendo vinavyofanywa na watu hao wanaojiita wanaharakati wa kutetea dini ya Uislamu na ndiyo maana kila kukicha tunaona hali ya kutishia amani ya nchi, misikiti ikitekwa, uhai wa viongozi wa dini ukitishiwa hadharani, viongozi wastaafu wakizabwa vibao hadharani kwa sababu za harakati za kidini," alisema.

Akitoa msimamo wa kanisa hilo, Mkuu wa Dayosisi ya Ushirika wa Meru, Askofu Paulo Akyo, alisema kilichotokea Mbagala katika wiki ya kumbukumbu ya Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ni aibu kwa Watanzania.

Alisema matokeo hayo, hayana tofauti na mauaji ya Kimbari, huku yakiwa ni matokeo ya mbegu ya magugu yaliyozaa matunda yaliyopandikizwa.

Kanisa lachomwa

Habari zaidi zinasema Kanisa la Faraja lililopo Yombo Makangarawe limevamiwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana na kuchomwa moto.

Akizungumza na MTANZANIA, Mchungaji wa Kanisa hilo, Peter Kusaga, alisema tukio hilo lilitokea usiku wa kumkia jana na moto huo umeteketeza mali zenye thamani ya Sh milioni 5.

DC TEMEKE

Naye Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema, ameto onyo kwa watu wanaojaribu kuvuruga amani wilayani humo.

Alisema Serikali inaendelea na kazi ya kuwasaka kwa udi na uvumba wahusika wa tukio hilo.

0 Maoni:

Post a Comment