Ndugu wanJF, Juzi juzi nimemsikia mchambuzi maarufu dr. Lwaitama akihojiwa kupitia Sibuka TV, pamoja na nondo nyingi alizotoa, nimefurahishwa na hoja ya kama mtu ni msafi anafanya nini ndani ya chama kichafu, chama ambacho kimetuletea umaskini wa kutupwa, mwanasiasa msafi iweje agombee kupitia chama ambacho kinanuka, na wananchi hawakitaki?

Mtaaluma huyo alienda mbali na kuiasa jamii iwapige chini wale ambao wanajipapambua kuwa ni wasafi huku wanashikiria mikoba ya chama kichafu. Hapa ndio hatari sana, maana mtu msafi atakaa vipi chama kichafu, alihoji mtadi huyo.

Ktk mambo mengi hili suala lilinigusa sana, hivi kweli iweje mtu msafi akae chama kichafu, hapa ndo nikawakumbuka kina magufuli, mwakyembe, sitta, kilango, filikunjombe, maige, shelukindo beatrice, january makamba na wengine wa aina hiyo.

Kama kweli hawa watu ni wasafi na bado wako chama kichafu, basi kunashida kubwa (wako mentally dehydrated) na ni ukweli kuwa wao ndo hatari sana kwa jamii ya kitanzania. Kwa uelewa wa sitta au makufuli au mwakyembe bado wanafanya nini huko kama kweli wao niwasafi??? why not to form a winning team na wasafi wenzao? Shida ipo hapo, Watanzania tuwakatae kama wasaliti ktk jamii.Usaliti zamani au kwa wenzetu walioendelea ni kosa kubwa sana, mtu mwenye akili timamu asingependa alifanye.

Kauli ya Lwaitama ilinikumbusha usemi wa mwanafalsafa mmoja unahusu unafiki katika jamii, it is not the bad people to blame, it is the good ones who opt willingly to remain silence while the bad people act against humankind.

TUWAPIGE VITA WATU HAWA MCHANA, USIKU, POPOTE NA DAIMA.

By:FikiliKwanza