Shughuli za uokozi zinatarajiwa kuanza tena leo asubuhi mashariki mwa Uganda ambako vijiji vitatu vilifunikwa na udongo kufuatia maporomoka ya udongo yaliyokumba eneo la Bududa.
Shirika la msalaba mwekundu nchini Uganda limesema kuwa zaidi ya watu 100 wamefariki dunia katika maporomoko hayo.
Zaidi ya nyumba kumi na tano zimezikwa kufuatia mvua kubwa iliyonyesha katika eneo hilo.
Shirika hilo limesema maafisa wake wanaendelea kuwatibu waliojeruhiwa katika mkasa huo, katika eneo hilo lenye rutuba la Bududa, linalokuza kahawa na lililopo karibu na mbuga ya wanyama ya mlima Elgon.
nyumba zimefunikwa futi16 chini
Mwandishi wa habari, Stephene Mulaa, aliyezuru eneo la tukio amesema kuwa, ''kufikia jana jioni hakuna mwili hata mmoja ulikuwa umepatikana, kwa sababu inakadiriwa kwamba miili ya watu na nyumba zilizofunikwa na udongo ziko zaidi ya futi kumi na sita kwenda chini''
0 Maoni:
Post a Comment