Mwigulu Mchemba Naibu Katibu CCM Bara,
Mbunge Jamhuri ya Muungano Tanzania


Mwigulu Mchemba mhusika mkuu Movie ya Rwekatare
Mwigulu Mchemba Mhusika Mkuu katika kashfa ya filamu inayodaiwa kuwa ya ugaidi ambaye amejipambanua na kutangaza hadharani kupitia:
  1. Chombo cha habari TV Desemba Mwakajana
  2. Mtandao wa Jamii Forums kiambatanisho cha nukuru JF hapo chini Jana tarehe 29/03/2013 hapo chini

Ameandika kwamba alikabidhiwa mkanda huo na mmoja wa viongozi wa Chadema, akiwa ni verified user member wa JF Mwigulu Mchemba amekiri kuhusika na mkanda huo, polisi kwa kutumia weledi unaotakiwa kisheria Mwigulu Mchemba ashikwe na kuunganishwa katika kesi hiyo kwani ndiye mwenye kuleta jawabu kamili namna alivyoupata mkanda huo, aliyempa na makandokando yake.

Kinyume cha kutofanya hivyo ni ushahidi movie hiyo kutengenezwa kwa ushirikiano wa huyu Mwigulu Mchemba na vyombo vya usalama ndio maana analindwa kutohusishwa katika kesi hii ingawa kuna ushahidi wa wazi kuhusika.

NB:
Hata vyombo vya dola vikiendelea kumkwepesha kwa kumlinda, taratibu na sheria za mahakama hatakwepa kuunganishwa katika kashfa hiyo kwani anaonekana ndiye shahidi maalum katika kesi hiyo kwa vile hajaonyesha siri kwani amejipambanua muda mrefu wa kutosha kuhusika na movie hii.


Mwigulu Nchemba


By king kan
Kama umejifunza uzalendo na utiifu kwa taifa. Prove your words by doing yafuatayo: 1. Saidia kueleza watanzania na polisi juu ya mkanda wa mauaji katika nyanja zifuatazo wewe uliupataje, nani alikupatia hiyo kopi na kwa nini hukutoa taarifa kwa vyombo vya dola na badala yake ulitumia media? 2. Uhalali wa elimu yako na jina lako ili tujue kama hukuiba fursa ya mtanzania mwingine ya kupata elimu? Kwa sasa nijibu kwanza hayo.

By Mwigulu Mchemba
King Swala liko mahakamani kumtaja aliyenipa itahatarisha maisha yake ila ni kiongozi wa chadema. Kuhusu elimu na jina mimi nilisoma mpaka darasa la tano nikaacha nikaenda kambini kuchunga mifugo nikarudi shule after 2 year nimefanya mtihani wa darasa la saba mwenyewe sijampoka mtu nafasi. Jina linawachanganya bure nilipewa la nesi aliyenipokea baada ya kuzaliwa home. Ndiye alikuwa akiitwa Mwigulu/Lameck. Mimi nilikuwa nikiitwa Mugulo. Mkanda nilipeleka vyombo vya usalama kabla ya media ila wao wananamna ya kuchunguza

Update

Kauli ya Tundu Lissu

Ukiacha sakata hilo ndani ya Chadema, Mnidhamu wa chama hicho, Tundu Lissu, yeye hataki kuuma maneno na hivyo ameamua kupasua jipu. Amesema ushahidi uliopatikana unaeleza kuwa siku chache baada ya kurekodi mkanda huo,
Mwigulu Nchemba alimtumia Ludovick Sh 50,000 kupitia mtandao wa Vodacom, hivyo anahoji zilikuwa za nini.
“Hivi leo Sh 50,000, si milioni Sh 5,000,000 au kumi ni Sh 50,000 tu zinasababisha amsaliti mtu wake wa karibu na kumsabishia alale Magereza?

Ludovick aisaliti familia iliyomsaidia
Lissu anasema anashangaa kusikia Ludovick ameamua kuisaliti familia ya Lwakatare kwa kuwa alikuwa ni mtu wa karibu wa familia hiyo, kwani Lwakatare na mkewe ndiyo waliosimamia na kufanikisha ndoa ya Ludovick. Amesema Ludovick pia ndiye aliyekuwa wakala wa Lwakatare katika kusimamia kuhesabu kura wakati akigombea ubunge mwaka 2010 jimboni Bukoba. Hata hivyo, Lissu anakiri kuwa Ludovick alikuwa mwanachama mtiifu wa Chadema na alikuwa katika kikosi cha Blue Guard, ila anahoji:
“Ninavyoijua afya ya Lwakatare ilivyo, asipokula tu inakuwa mgogoro unafikiri kesho Ludovick ataonekana vipi kwa watoto wa Lwakatare,” amesema. Lissu amesema kupitia mkakati aliouita wa ‘kishamba’, kamwe Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakitaiangusha Chadema bali ni kuzidi kukipa umaarufu siku za usoni.

Ludovick alivyorekodi mkanda
Amesema Desemba 28 mwaka jana saa 5 asubuhi Ludovick alikwenda nyumbani kwa Lwakatale na saa 5:59 na
akiwa hapo alimpigia simu Nchemba kwa namba iliyoorodheshwa kwenye kitabu cha Bunge kutaarifu kuwa amefika. Ameongeza kuwa kwa kuwa Ludovick alikuwa kama mtoto wa nyumbani, aliingia nyumbani kwa Lwakatare muda wowote na kukaa sehemu yeyote, hivyo siku hiyo ndiyo aliyoamua kufanya kazi hiyo kwa kumuliza Lwakatare maswali ya mtengo.

Amesema katika mkanda huo inasikika sauti ya Ludovick ikiuliza maswali ambayo yanatengeneza jibu, ambayo hutumika kama mtego wa kumtega muulizwaji ili atoe jibu analotaka muulizaji. Lissu amesema, hata hivyo, anashukuru majibu yaliyotolewa na Lwakatare hayakuwa kama muulizaji alivyotaka. Amesema kuwa iwapo angejibu kama Ludovick alivyotaka Chadema ingekuwa na hali mbaya na kesi hiyo ingekuwa ngumu kwao.

Historia ya Ludovick utata
Wakati mahakama ikisubiriwa kusikiliza na kutoa uamuzi wa mashitaka yaliyofunguliwa dhidi ya watuhumiwa, habari zilizopatikana zinasema Ludovick amekuwa akiishi maisha ya “aina yake”.


  • Habari za uhakika zinasema kwamba mtuhumiwa huyo amepata kupewa hifadhi katika familia moja mjini Morogoro, baada ya kujitambulisha kuwa ni yatima. Kwa maelezo yake, aliomba msaada wa kusomeshwa, na akafanikiwa kupelekwa katika Chuo cha Ualimu Morogoro.
  • Imeelezwa kwamba katika kipindi hicho, alifahamiana na mtu mmoja mwenye asili ya Mkoa wa Mara (jina tunalo), ambaye alimwezesha kupata hifadhi nyumbani kwa mmoja wa viongozi katika mhimili mmoja hapa nchini (jina tunalihifadhi kwa sasa).
  • Hapo alieleza kwamba alikwama kusoma seminari kutokana na kufiwa na wazazi. Imeelezwa kwamba, akiwa nyumbani kwa msamaria mwema huyo, siku moja, usiku wa manane, aliruka ukuta na kutokomea, lakini aliweza kurejea saa 9:30 usiku.
  • “Baada ya kutoka tulimweleza bosi wetu, akaamua tukae nje tusubiri tuone kama atarudi. Kweli, alirudi 9:30 usiku, ajabu ni kwamba ukuta ulikuwa mrefu sana, lakini aliweza kuruka kwa namna ambayo sote tulishangaa.“Bosi wetu kuona hivyo akaamua kumfukuza. Lakini kabla ya hapo alimhoji na yeye akasema hajui namna anavyoweza kuruka ukuta, akasema ana matatizo ya akili,” amesema mmoja wa walinzi.
  • Habari nyingine zimesema kwamba akiwa Morogoro aliweza kuongoza ibada kadhaa za mazishi za madhehebu Katoliki. “Hatukumsikia tena baada ya kutoka Morogoro hadi tulipopata taarifa kwamba anasoma DUCE jijini Dar es Salaam,” kimesema chanzo chetu.


Update
Mwigulu akiri kuhusika video ya Lwakatare

  • HATIMAYE Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Mwigulu Nchemba, amekiri kuhusika na video inayomwonesha Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare.

Nchemba amekuwa akitajwa na viongozi wa CHADEMA kuwa anahusika kutengeneza video hiyo, kwa kuwa aliwahi kutamba wakati akihojiwa na kituo kimoja cha televisheni kuwa anayo video inayowaonesha viongozi wa chama hicho wakipanga mauaji.

Hata hivyo, tangu Nchemba atoe kauli hiyo Januari mwaka huu, Jeshi la Polisi lilikaa kimya hadi Machi 12 lilipomkamata na kumhoji Lwakatare, siku moja baada ya video hiyo kuwekwa kwenye mtandao wa You tube na mtu anayejiita ‘Bukoba Boy’.


Akizungumza na gazeti hili kwa simu jana, Nchemba alikiri kuwa ndiye aliyeipeleka video ya Lwakatare polisi na kwamba alifanya hivyo baada ya kuripoti kuandikiwa ujumbe wa simu wa kutishiwa maisha na baadhi ya viongozi wa CHADEMA.
“Niliwapelekea mimi hiyo video polisi na wakati nasema kwenye televisheni nilikuwa tayari nimewapa. Na pale nilisema makusudi baada ya Zitto Kabwe kudai kuwa mwaka jana kulitokea mauaji mengi, ndipo nikataka kumuonesha kuwa chama chake kinahusika na mikakati hiyo,” alisema.


Alipoulizwa aliipataje video hiyo na kwanini hajahojiwa polisi ili kutoa uthibitisho wa uhalali wake, Nchemba alisema: “Kuna msamaria mwema aliniletea.”
Nchemba alipobanwa ana uhakika gani kama video hiyo ina ukweli, alijibu kuwa: “Ile huhitaji akili kubwa kutambua uhalisia wake. Suala la Lwakatare CHADEMA wakubali tu na wajitokeze hadharani kwenye makanisa na misikiti, watubu na kuomba radhi kwa umma.”


Mchemba atoa siri za mahojiano Polisi na Rwekatare
Hata hivyo katika kile kinachoweza kuongeza mashaka ya Nchemba kuhusishwa kutengeneza video hiyo, alikwenda mbali zaidi akitoa hata siri za polisi, akisimulia maelezo aliyodai kuwa ndiyo yalitolewa na Lwakatare wakati akihojiwa na polisi.
“Pale video inaonesha ni nyumbani kwake, tena jikoni na hilo amekiri katika maelezo yake polisi. Pia amekubali kuwa siku hiyo alipiga chafya kama inavyoonekana. Sasa wewe mwandishi unatetea nini wakati yeye amekiri polisi kila kitu kilichomo mle,” alisema.

Maelezo ya Nchemba yalionekana kumtia hofu mmoja wa mawakili wa Lwakatare, ambaye alikuwepo wakati wote wa mahojiano polisi, Nyaronyo Kicheere, akidai kuwa ni wazi jeshi hilo linafanya kazi ya propaganda za CCM.
“Nchemba hakuwepo wakati Lwakatare akihojiwa na hata baadhi ya wanasheria katika kesi yake ya ugaidi inayomkabili hawajui alichokisema polisi, sasa huyo amepata wapi siri za polisi kama si mchezo unachezwa?” alihoji.

Kuhusu mahusiano yake na mshtakiwa wa pili katika kesi ya Lwakatare, Ludovick Joseph, ambaye anadaiwa na baadhi ya watu kuwa ndiye aliyerekodi video hiyo, Nchemba alisema walifahamiana kupitia mtandao wa kijamii wa facebook.
Alipotakiwa kufafanua ukaribu wao hadi kufikia hatua ya kumtumia fedha kwa njia ya M-Pesa kupitia simu yake, Nchemba alisema: “Mimi nilimtumia kama ninavyowapa watu wengine hata wa CHADEMA. “Mimi sijui kama Ludovick ndiye alirekodi video hiyo, wala sikuwahi kumtuma kufanya hivyo na fedha niliyomtumia si kwamba nilikuwa nikimlipa ujira. Kwani unaweza kumpa mtu sh 50,000 tu kwa kazi hiyo?” alihoji.


Tanzania Daima lilipotaka kufahamu kama anahusika kushirikiana na vyombo vya dola kuwarubuni baadhi ya vijana wa Makao Makuu CHADEMA kwa fedha ili watumike kutoa ushahidi wa kumwangamiza Lwakatare mahakamani, Nchemba alisema: “CHADEMA haijawahi kuongoza serikali, hivyo hawajui mikono ya serikali.”


Alipotakiwa kufafanua kikao baina yake na vijana hao kilichofanyika katika Hoteli ya Sea Cliff ya jijini Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi uliopita na kisha kuwatumia fedha kwa njia ya M-Pesa, Nchemba aling’aka na kuuliza: “Hiyo Hoteli ya Sea Cliff iko wapi? Maana sipajui na sijawahi kufika.”
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Mkurugenzi wa Mambo ya Katiba wa CHADEMA, Tundu Lissu, alifichua njama zinazofanywa ili kutengeneza ushahidi wa uongo kwa ajili ya kuutumia katika kesi ya ugaidi inayomkabili Wilfred Lwakatare.


Lissu alidai kuwa njama hizo zinafanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama na ujasusi ili kutumia ushahidi huo mahakamani dhidi ya Lwakatare.
Alisema kuna baadhi ya vijana wa CHADEMA wa Idara ya Ulinzi na Usalama wanaopewa fedha na kuahidiwa kufundishwa namna ya kuzungumza katika kesi hiyo ya Lwakatare. Lissu alisema kuna baadhi ya vijana wakiongozwa na Saumu Mulugu, ambaye alifukuzwa kazi CHADEMA mwanzoni mwa mwaka jana, wamepokea fedha kutoka kwa kigogo mmoja wa CCM (jina linahifadhiwa) ili kufanikisha mpango huo.


Lissu alisema hadi sasa vijana hao wameshapewa sh 400,000 ili wakubali kwenda kufundishwa jinsi ya kuzungumza mahakamani kuwa CHADEMA ni chama cha kigaidi, kwamba Lwakatare alipanga mikakati ya kigaidi.
“Awali walipewa sh 400,000, wakapewa tena sh 300,000, pia wakapewa sh 35,000 mara mbili. Na fedha zote hizi walikuwa wanapewa kwa njia ya M-Pesa,” alisema Lissu. Alidai kuwa Saumu ndiye anayeratibu mpango wote kati ya Jeshi la Polisi na vijana hao wa CHADEMA kwa kuwarubuni kwa fedha.

Alisema vikao baina ya vijana hao wa CHADEMA na Saumu vimewahi kufanyika mara kadhaa katika moja ya hoteli maarufu nchini juu ya mambo ya kwenda kuzungumza kwenye vyombo vya habari au mahakamani kwenye kesi ya Lwakatare.

Tanzania daima yanasa mawasiliano ya Saumu na wenzake
Siku moja baada ya madai ya Lissu, gazeti hili lilimnasa Saumu akiwa anawasiliana na wenzake, huku akiwatuhumu baadhi yao kuwa ndio waliovujisha siri kwa Lissu.
Vilevile alionekana akiwasiliana na kigogo mmoja wa CCM ambaye alikuwa akimwita ‘mkuu’ huku akimsomea baadhi ya taarifa zilizoandikwa magazetini jana yake kuhusu kuvuja kwa siri zao.


Saumu akiwa katika grosari karibu na baa maarufu kwa jina la Kwa Kimaro, jirani na eneo la Benki Kuu ya Damu Salama, Mchikichini jijini Dar es Salaam, alisikika akiwalalamikia wenzake kwa kumsaliti na kuvujisha mkakati wao kwa Lissu.
“Kwanini mmelikisha siri zetu kwa Lissu hadi amejua tulikutana katika hoteli ya kifahari na Mwigu…? Sasa nitawaonesha, maana laki tano zenu ninazo mimi. Siwapi bali nitazitumia kujilinda,” alitamba.


Saumu ambaye alikuwa akizungumza kwa sauti kubwa ya ghadhabu kupitia simu, aling’aka: “Nyie kwanini mmeniuza kwenye ishu ambayo tumeipanga wote?”
Baada ya kupokea maelekezo kutoka kwa ‘mkuu wake’ aliendelea kupiga simu akimlalamikia mtu ambaye hakumtaja, kuwa alikuwa amezima simu yake makusudi kwa kuwa ndiye alivujisha siri zao kwa CHADEMA. “Mimi sitakubali na nimehakikishiwa na bosi wetu kuwa huyo aliyetusaliti tutatumia wale askari kumwekea hata unga. Haiwezekani fedha tumepokea za kwanza, za pili na tatu kwanini tuuzane dakika za mwisho?” alidai Saumu huku akiendelea kugida bia yake.


Huku akihaha huku na kule, Saumu alikuwa akiwapigia simu baadhi ya madereva wa CHADEMA makao makuu na kuwaomba simu za baadhi ya watu, na hata wakati mwingine kuwafokea akidai ndio waliofichua siri hiyo.
Hata hivyo, baada ya kutilia shaka nyendo za chanzo chetu kudaka siri zake, ghafla alitokomea na kuzima simu zake mara moja kwani hata alipotafutwa baadaye hakupatikana hadi leo.