Naibu Katibu Mkuu wa CDM Zitto Kabwe jioni hii anatarajiwa kutikisa mji wa Bagamoyo katika kampeni za kumnadi mgombea udiwani wa CDM katika kata ya Magomeni.

Mgombea udiwani huyo wa CDM anaungwa mkono na wananchi na kuna uwezekano mkubwa wa kushinda katika uchaguzi utakaofanyika jumapili wiki hii.

Wakati Zitto yuko Bagamoyo viongozi wakuu wa chama hicho wamejichimbia maeneo mbalimbali nchini kuhakikisha CDM inapata ushindi mkubwa katika kata 29 zitakazofanya uchaguzi.Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe kwa wiki nzima yuko mikoa ya kusini huku Katibu mkuu wake Dr Wilbroad Slaa amejichimbia Kanda ya ziwa kwa wiki mbili sasa.

Mjumbe wa Kamati Kuu Godbless Lema akisaidiwa na Kamanda Henry Kilewo yuko Kanda ya Kaskazini huku Mkurugenzi wa Mafunzo na operesheni Benson Kigaila akipambana Kanda ya Kati.

Makamanda wengine walioko mstari wa mbele wa mapambano ni Alphonce Mawaazo na Ally Bananga wakipigania Kata za Mkoa wa Morogoro.