Wednesday, October 24, 2012

Kwa watu wa mkoa wa Mara

 

Ni matumaini yangu kuwa mpo salama,kwa upande wangu namshukuru Mungu.
Kwanza kabisa ni-declare interest kwamba mimi ni wa mkoa wa Mara,wilaya ya Serengeti,tarafa ya Ngoreme,kata ya Kenyamonta.

Nina machache leo ya kuzungumza na wana-Mara wenzangu kuhusu mkoa wetu.

Mkoa wa mara ulikuwa na kasifa hivi hasa kalikoletwa na mwl nyerere,kwamba baba wa taifa kutoka mara.Zaidi ya hapo tunabaki na sifa za kijinga tu ambazo kimsingi haziujengi mkoa wetu bali kuudidimiza na sisi tunabaki kuchekelea tu huku nyumba inaungua.

Mji mkuu wa mkoa wa Mara ni Musoma mjini,mtakubaliana nami kuwa mji ule umekuwa kama mtoto aliyesumbuliwa na kwashiakoo kwa muda mrefu,yaani umedumaa,hauna mabadiliko chanya tangu nianze kuwa na ufahamu,bali unakuwa kwa kwenda nyuma.

Wilaya ya Serengeti na Taarime zimekuwa zikisifika kwa fujo na watu wake eti kuitwa majasiri,hizo ni sifa za kijinga na wanaotuita hivyo wanafanya makusudi kutudumaza kimaendeleo.

Wilaya ya Serengeti,Musoma vijijini,na Bunda zinaelekea kugeuka jangwa.Wachoma mikaa wamefyeka kupita kiasi,huku watendaji wa serikali wakiwepo tu.Hawana uchungu maana wengi wao ni wa kupita tu,sisi wakudumu ndo tumeamua kujitengenezea jangwa.


Ujasiri wetu uko wapi kama si ujinga,tuna sehemu kubwa ya ziwa victoria,samaki wanavuliwa,minofu inatolewa,kisha watu wetu wanakula mifupa(mapanki),huo ndio ujasiri.

Mbuga ya Serengeti kwa asilimia kubwa ipo mkoani Mara,lakini kupata nyama kama kitoweo kwa siku hizi kupitia mbuga ni dhambi ambayo adhabu yake ni kupigwa risasi hadi kufa.Kama mtakumbuka zamani kulikuwa na kipindi fulani kwa mwaka wanaruhusu wananchi kuwinda kwa ajiri ya kitoweo.Hakukua na tatizo,wala hatujawahi kusikia wanyama wamepungua,ilikuwa ecosystem ya kawaida kwani sisi ni sehemu ya mbuga.Mfumo umefutwa,mbuga sasa iko na VIP,ukitaka kutangulia mbele ya haki katiza mbugani.Tumebaki kuangalia tu,wamefika mahali twiga wanabebwa na kupelekwa nje,eti mkoa wa Mara ni majasiri,sifa za kijinga.


Madini ya dhahabu yapo kwa wingi mkoani Mara,kuna Nyamongo,Buhemba,Park Nyigoti,Majimoto japo kwa uchache.Tunafaidije kama si kusaidia mkoa wa Mara kuwa na takwimu ya juu kwa virusi vya ukimwi na ukimwi(7.8%)
Eti mkoa wa Mara ni majasiri,sifa za kijinga.


Mkoa umekosa chuo cha maana cha utalii na Hotel management,vipo vya hovyo tu.Vyuo vya maana vipo Arusha na hivyo waajiriwa wengi wa hotel za mbugani wanatoka Arusha,Mara tunabaki kulalamika tu.Eti sisi ni majasiri,sifa za kijinga hizi.

Rais analazimisha kupitisha barabara ya lami mbugani kwa maslahi yake binafsi(Kwa sababu ana hotel mbugani),watu wa mkoa wa mara tumenyamaza tu,wakati tunafahamu madhara yake.Eti majasiri,ujinga huu.

Mbuga ipo kwetu,ukipita barabara ya mbugani unalazimika kulipa ada ya kupita mbugani,kama vile wewe ni mtalii.Huu ni uhuni tunafanyiwa,udau wetu juu ya hii mbuga upo wapi.Kwanini ulazimishwe kukatwa pesa hiyo wakati hukuwa na mpango wa utalii.Eti Mara majasiri.

Tukiendelea kubweteka na sifa hizi za kijinga kuna wakati utafika Mara itatambulishwa kama sehemu ya Arusha,"AMINI NAWAAMBIENI"

Waliotufikisha hapa wanajulikana,imefika wakati Mkoa wa Mara kuanzisha muungano wa vijana wa MKOA.Vijana wa Mara wakiwa na sauti moja,wanaweza kupanga vipaumbele vya mkoa,na mwanasiasa yeyote atakaetaka ridhaa yetu aonyeshe nia ya dhati kabisa ya kushughulikia vipaumbele hivyo.Vijana tunaweza kufanya hivyo,lakini pia umefika wakati wa sisi vijana kuufanyia kitu mkoa wetu pamoja na taifa kwa ujumla.

Nilikuwa naongea na mmoja wa wabunge wa mkoa wa Mara eti anasema mkoa umedhorota kwa sababu vijana wake wengi ni walevi,so what?ana maanisha hakuna mabadiliko?kwanini aliomba uongozi.

Naomba tupeane maoni juu ya mkoa wetu,tukosoane kwa kujenga na ikiwezekana tuje na harakati mpya za kuujenga mkoa wetu.

Mods kama kuna madainayoendana na hii ilishatolewa naomba msii-combine,nataka kupata maoni ya wadau.
Chanzo:Jukwaa la siasa By Mwita Maranya.

0 Maoni:

Post a Comment