-
Amirijeshi Mkuu, Jakaya Kikwete akimwapisha Luteni Jenerali Samuel
Albert Ndomba (kulia) kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi
wa Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu leo jijini Dar es salaam.
Meja Jenerali Ndomba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Luteni Jenerali
Abdulrahaman Shimbo aliyestaafu utumishi jeshini kwa Umri.
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu wa Majeshi
ya Ulinzi na Usalama Dkt. Jakaya Kikwete akimwapisha Meja Jenerali
Raphael Mugoya Muhuga (kulia) kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)
leo Ikulu jijini Dar es salaam
Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi
nchini Jenerali Devis Mwamunyange (kushoto) na maofisa wa Jeshi Luteni
Jenerali Samuel Ndomba, Mnadhimu Mkuu wa JWTZ (wa tatu kutoka kushoto)
na Meja Jenerali Raphael Mugoya Muhuga mkuu wa JKT walioapishwa leo
Ikulu jijini Dar es salaam.
-
Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wizara ya
Ulinzi na Maofisa wa JWTZ na Jeshi la Kujenga Taifa leo mara baada ya
hafla fupi ya kuwaapisha Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Samuel Ndomba na Mkuu wa JKT Meja
Jenerali Raphael Muhuga.

-
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Devis Mwamunyange
(kushoto) akimweleza jambo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
Jakaya Kikwete (kulia) katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es
salaam.Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki
(katikati).
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Luteni
Jenerali Samuel Albert Ndomba akiongea na waandishi wa habari mara baada
ya kuapishwa leo jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akiwa na
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kulia) akiwaeleza jambo viongozi wa Jeshi la
Polisi nchini Inspekta Jenerali Saidi Mwema, mkuu wa Jeshi la Polisi (wa
pili kutoka kulia) na Paul Chagonja kamishina wa Oparesheni. Kulia ni
Mkuu wa Majeshi Jenerali Devis Mwamunyange.

-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi
ya Ulinzi na Usalama Dkt. Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Maofisa
waandamizi wanawake wa JWTZ leo Ikulu jijini Dar es salaam. Kulia ni
Meja Jenerali Lilian Kingazi (Kulia) na Meja Jenerali Grace Mwakipunda
(kulia). Picha zote na Aron Msigwa – MAELEZO.
Kuhusu:
0 Maoni:
Post a Comment