Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mhe:Freeman Mbowe. CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeitaka Serikali kuacha kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kuangalia upepo wa kisiasa, ili kuepuka kuwapa wananchi mateso na umaskini.
Pia kimewataka wanachama wake, kudai haki zao kwa amani badala ya kutumia nguvu zinazoweza kusababisha umwagaji wa damu.
Rai hizo zilitolewa juzi kwa nyakati tofauti na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Makamu wake wa Zanzibar, Said Issa walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari.
Mbowe kwa upande wake, alitoa rai hiyo kupitia hotuba yake iliyosomwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Tanzania Bara, Zitto Kabwe, katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Mnadani Mjini Katesh.
Zitto na wabunge wengine wa Chadema, walipita katika kijiji hicho wakitokea wilayani Rombo.
Katika hotuba hiyo, Mbowe alisema Chadema imedhamiria kufa ikiwa katika harakati za kupigania haki za wananchi ikiwemo ya kumiliki ardhi na kupinga uonevu wa aina mbalimbali, unaofanywa na baadhi ya watawala wasiokuwa
waaminifu.
“Chadema imejipanga ili kuhakikisha kuwa haki za wananchi zinapatikana na wanatumia rasilimali zao kujinufaisha kiuchumi kuliko ilivyo sasa wanapoambulia kula makopa,” alisema Mbowe kupitia hotuba yake.
Tuesday, August 14, 2012
Chadema: Tudai haki bila kumwaga damu
Imeandikwa 2:55 PM na Steven Elias
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Maoni:
Post a Comment