wanajamvi mmemsikia Dk. Slaa akieleza jinsi CUF inavyotegemea serikali hata kugharamia vikao vya chama. Hapa upinzani wa kweli unakuwa mashakani. Msikieni Slaa akiunguruma

"Dk. Slaa atoboa siri ya CUF
Naye Dk. Slaa alitoboa siri ya namna CUF ilivyoamua kuwa sehemu ya utawala, baada ya kufichua barua mbili zikiomba fedha kwa ajili ya kuhudumia chama na safari za kifamilia za Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar.Alisema barua ya kwanza ya Katibu Mkuu wa CUF Maalimu Seif kwenda serikalini inaomba kuwezeshwa kufanyika kwa mkutano wao wa chama kwa siku tatu katika eneo la Bagamoyo kwa gharama za sh milioni 34.Dk. Slaa alisema barua ya pili ni ile inayoomba dola za Kimarekani 10,000 kwa ajili ya nauli ya kwenda Nairobi Kenya kwa mke wa Maalim Seif kwa safari ya kifamilia, ikiwa ni sawa na dola 1,000 kwa siku.Aidha Dk. Slaa alisema katika taarifa hiyo inaonyesha pia kuna fedha za dharura kwa ajili ya matumizi ya Makamu wa Rais ambayo ni dola 3000 na kudai kuwa huo ni ufisadi usioweza kuvumiliwa na wapenda haki.Alisema kwa mfumo huo wa CUF kutegemea hata katika mikutano yake ya chama fedha za serikali, ni ushahidi wa waziwazi kuwa inafanya kila kitu kwa kuongozwa na serikali ya CCM."