Takriban asilimia tisini ya wanwake katika kijji kimoja inasemekana wameondolewa mfuko wao wa uzazi
        Wakereketwa wa haki za 
kibinadamu wanasema kuwa maelfu ya wanawake wamekuwa wakiondolewa mfuko 
wa uzazi kwa ulaghai ambapo wanadanganywa kuwa watashikwa na saratani 
iwapo hawafanyiwi hivyo katika kliniki za kibinafsi.
Ifuatayo ni taarifa ya Jill Mcgivering ikisimuliwa na Wanyama wa Chebusiri.
Kuongezeka kwa visa vya wanawake 
kuondolewa mfuko wa uzazi, ni kutokana na ongezeko la kliniki na 
hospitali za kibinafsi katika miaka ya hivi karibuni.
Zote hizo zinajaza pengo la mfumo duni wa serikali hususan katika maeneo ya vijijini.
Wanaharakati wanataka hospitali hizo kuchunguzwa
 na hata kuwekewa sheria za utenda kazi ili kuhakikisha kuwa 
haziwanyanyasi akina mama maskini.
Daktari Narendra Gupta anayefanya kazi katika 
shirika moja lisilo la kiserikali, Prayas anasema kuwa madaktari wa 
kibinafsi, wameona fursa ya kutengeza pesa kwa haraka.
Anaelezea kuwa kuna mbinu nyingi tu ambazo, 
mfuko wa uzazi unaweza kuondolewa bila upasuaji, na kwamba hiyo inapaswa
 kuwa tu njia ya mwisho katika matibabu yoyote.
Mmjoa wa wanawake walioondolewa mfuko wao wa uzazi
Baada ya kuondoa mfuko wa uzazi huwa ni vigumu kuthibitisha kuwa operesheni hiyo haikuwa budi kufanywa.
Lakini jambo la kushangaza ni kuwa wasichana 
wadogo wanaondolewa mfuko huo baada ya madakrati kuwatisha kuwa watapata
 saratani ikiwa hautaondolewa.
Waziri wa ustawi wa vijijini Jairam Ramesh, 
anasema kuwa changamoto kubwa ni kuwa mfumo wa serikali umeporomoka na 
kwamba watu hulazimika kwenda katika hospitali za kibinfasi,
Anasema kuwa kwa hilo watu hulazimika kutumia pesa nyingi sana na hata kupata matibabu wasiyoyahitaji
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

0 Maoni:
Post a Comment