TAMKO LA CHADEMA KUHUSU KUTEKWA KWA DKT: STEVEN ULIMBOKA. 
Ndugu wanahabari kwanza asanteni kwa kuitikia mwito wetu leo na kwa  ushirikiano mnaotoa kwa Watanzania katika majukumu yenu ya kila siku  katika kuitumikia jamii. Kuna masuala mawili tungependa kuzungumza mbele  yenu leo;
Kwanza; kwa namna ya pekee, Chama cha Demokrasia na  Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya kutekwa,  kuteswa na kuumizwa vibaya kwa Kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari nchini  Dkt. Steven Ulimboka jijini Dar es salaam. Tukio hili limetukumbusha  mambo mengi ambayo yamekifanya chama chetu kitafakari kwa kina suala  zima la mgomo wa madaktari unaoendelea nchini. Kama tulivyowahi kusema  mara kadhaa kuwa ni bahati mbaya sana kuwa madaktari wetu ambao kwa  hakika ni wachache sana, wanalazimika kutumia haki yao ya kugoma katika  kudai maboresho ya msingi kwenye sekta ya afya, jambo ambalo linagharamu  maisha ya watu hususani wa kawaida (walalahoi) ambao matibabu yao  hutegemea hospitali za umma.
CHADEMA inaamini kuwa moja ya  majukumu ya msingi ya serikali yoyote makini ni wajibu wa kulinda haki,  mali na usalama wa kila raia na pia kuhakikisha kuwa huduma muhimu za  jamii zinapatikana wakati wote kwa nchi nzima. Tukio la kutekwa nyara  kwa kiongozi wa madaktari, Dkt. Ulimboka, si suala dogo wala la mzaha na  haliwezi kuisha kwa MALALAMIKO tu, ya sisi wapinzani, wanaharakati na  serikali yenyewe. Hapa ni lazima watu wenye wajibu wa kuhakikisha  usalama huo wa raia wawajibike, hasa katika kutuambia ukweli wa nani  aliyehusika na UGAIDI huu afahamike na hatua zichukuliwe dhidi yake.
Tukio  hili linatukumbusha njama mbalimbali ambazo zimekuwa zinafanywa na  serikali dhalimu katika maeneo mengine duniani dhidi ya wapigania haki  au wale wote wanaotoa mawazo mbadala dhidi ya watawala. Lakini pia  katika nchi yetu hii leo, yapo mauaji ambayo yana kila harufu ya  serikali, vyombo vyake na chama tawala kuhusika. Mfano mauaji ya  kijanaMbwana Masoud, aliyeuawa huko Igunga mwaka Oktoba 2011, baada ya  kutekwa na kuteswa.
Mfano mwingine ni mauaji ya Kiongozi wa  CHADEMA Kata ya Usa River,Msafiri Mbwambo, huko Arumeru Aprili 2012,  viongozi na wanaharakati kubambikiwa mashtaka ya uongo sehemu mbalimbli  nchini, kuzingirwa kwaWabunge wa CHADEMA huko Mwanza, kisha wakapigwa na  kuumizwa vibaya,wanafunzi wa vyuo vikuu nchini, hususan viongozi wao,  kunyimwa haki zao za kusomeshwa na kufunguliwa mashtaka yasiyo na msingi  kwa sababu ya misimamo yao katika kudai haki, n.k.
Lakini pia  tukio hili linakumbushia matukio ya namna hii ambayo yamehusishwa na  vyombo vya dola pamoja na CCM wakati wa chaguzi ndogo katika maeneo  mbalimbali mathalani huko Kiteto, Biharamulo na Busanda ambako mpaka leo  pamoja na kuwepo kwa viashiria vyote kuwa serikali, kwa maana ya dola  ilihusika katika matukio ya namna hii ili kukisaidia CCM kushinda  uchaguzi, hakuna hatua zozote zilizochukuliwa zaidi ya polisi kukalia  majalada hayo mpaka leo.
Yote hayo hapo juu yanaimarisha msimamo  wetu kuwa ni LAZIMA serikali iwe na jibu la kutekwa, kuteswa na kuumizwa  vibaya kwa Dr. Ulimboka.
Na katika hili CHADEMA tunaweka msimamo  kuwa serikali haiwezi kuaminika katika kufanya uchunguzi, wala Jeshi la  Polisi pia haliwezi kuwa na uhalali wa kufanya hiyo kazi. Mpaka sasa  kwa mazingira yaliyopo, serikali ni mtuhumiwa katika tukio la kutekwa,  kuteswa na kuumizwa sana kwa Dkt. Ulimboka. Ni kanuni ya msingi sana  katika dhana ya uongozi bora, kuwa mtuhumiwa hawezi kujichunguza  mwenyewe.
Wakati ambapo Watanzania wote tunaoitakia heri nchi  yetu, tukiendelea kumwombea Dkt. Ulimboka katika wakati mgumu wa maumivu  makali aliyonayo apone haraka, CHADEMA kinaitaka serikali kutohusika  kwa namna yoyote katika uchunguzi wa tukio la Dkt. Ulimboka.
Ili  waliohusika wapatikane na kuwajibishwa, tunataka iundwe tume huru,  itakayojumuisha watu wanaoaminika kutoka kada mbalimbali, ili ufanyike  uchunguzi huru juu ya suala hili ambalo ni dhahiri limeibua taharuki  nyingine katikati ya taharuki kubwa ya mgomo wa madaktari ambao unazidi  kushika kasi kwa sababu ya serikali kutowajibika ipasavyo kwa wananchi  walioiweka madarakani. Kuundwa kwa tume huru kuchunguza matukio au vifo  tata kila inapotokea, imekuwa ni rai yetu mara kwa mara ili serikali  ioneshe uongozi bora kwa vitendo.
Mbali ya kuwa suala hili  linahusu maisha ya binadamu ambayo hayana thamani ya kitu kingine  chochote, bado pia ni kitendo kinachozima demokrasia na kuhatarishaamani  ya taifa.
Kuhusu mgomo wa madaktari
Ndugu wanahabari  suala la pili; lazima sasa mgomo huu wa madaktari unaoendelea umalizike  kwa wananchi ambao ndio wanaoathirika, kuingilia kati iliserikali  imalize mvutano na madaktari. CHADEMA kinaona suala hili kuwa zaidi ya  “siasa”. Ni suala linalohusu maisha ya watu. Tunatoa mwito kwa watu wote  wenye mapenzi mema kuungana katika kushinikiza mgomo wa madaktari  kupatiwa suluhisho la kudumu ili kunusuru maisha ya Watanzania, hasa  wasiokuwa na uwezo wa kutibiwa nje ya nchi kama viongozi wao. Dawa ya  mgomo huu iko ndani ya uwezo wa serikali; isipokuwa tuhaina nia ya kweli  na dhati kutatua tatizo hili kwa manufaa ya wananchi. Kwa kuwa serikali  ni ya wananchi na serikali inawajibika kwa wananchi katika masuala  yote, ikiwemo kuhakikisha huduma za jamii zinapatikana, ni lazima sasa  wenye nchi hawa waoneshe msimamo wao katika suala hili. Tunawaomba  Watanzania kusimama kuiwajibisha, ikiwa Serikali ya Rais Kikwete chini  ya CCM, itaendelea kupuuza na kufanya mzaha katika suala hili  linalohatarisha amani na utulivu wa taifa.
Kama Serikali ya Rais  Kikwete itaendelea kupuuza, hata baada ya msimamo wa wananchi wa kuitaka  iwajibike kutatua tatizo hili, basi serikali hii itakuwa imeongeza  idadi ya viashiria vinavyoikosesha uhalali wa kuongoza.
Ndugu  wanahabari, kwa kipekee kabisa tunawasihi Watanzania ambao ndiyo  waathirika wakubwa wa mvutano kati ya serikali na madaktari,  uliosababisha mgomo unaoendelea, wamtake Rais Jakaya Mrisho Kikwete  amalize mgomo huumara moja kuzuia madhara makubwa kwa maisha ya  binadamu.
Tunasema hivyo kwa sababu, katika mgomo wa awali,  Januari/Februari, baada ya wasaidizi wake, akiwemo Waziri Mkuu Mizengo  Pinda kushindwa kuutatua, suala hili lilifika kwa Rais Kikwete, ambaye  alikutana, kujadiliana na kufikia mwafaka na madaktari.Baada ya hapo  aliwatangazia Watanzania wote kupitia ‘wazee wa Dar es Salaam’, kuwa  mgomo umekwisha. Rais Kikwete aliahidi pia kuwa hakutakuwa na mgomo wa  madaktari tena. Sasa tunamtaka Rais Kikwete atoke hadharani tena  awaambie Watanzania vitu gani alikubaliana na madaktari, ametekeleza  yapi na mangapi ambayo hayajatekelezwa mpaka sasa, kiasi madaktari  wameamua kugoma tena,huku wananchi wakiumia. Serikali haiwezi kukwepa  kuwajibika kwa madhara yoyote yanayotokea kwa maisha ya binadamu,  kutokana na mgomo wa madaktari.
Tunasisitiza huu ni wajibu wa  Rais Kikwete kwa Watanzania, kwa sababu wanajua suala hili lilishafika  kwake. Kinyume na hapo Watanzania wataendelea kujua wanaye rais wa namna  gani katika kusimamia masuala ya msingi yanayoamua hatma yao, mtu mmoja  mmoja na kama taifa.
Kwa sababu Mhimili wa Bunge ambao ndiyo  mwakilishi wa wananchi, ulipaswa kuwa tegemeo na kimbilio katika kuokoa  maisha ya watu, umeonekana kuwa na meno ya plastiki na kushindwa  kuwaokoa Watanzania, tunatumia fursa hiikuwataka Watanzania wote  watimize wajibu wao wa kuitaka serikali na Rais Kikwete kumaliza mgomo  huu.
Ndugu wanahabari mwisho tunasema kuwa Serikali isiyoweza  kuwahakikishia wananchi wake usalama na upatikanaji wa huduma zingine  muhimu za jamii, mathalani; afya, elimu, maji, umeme n.k, ni serikali  inayopoteza uhalali wa kuongoza.
Imetolewa leo Juni 28, 2012 Dar es Salaam na;
Singo K. Benson
Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo-CHADEMA
Kny. Katibu Mkuu 
Kuhusu
Chat nami hapa
Zinazosomwa sana
- 
Bi:Angela Merkel Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amekataa shinikizo la kujumuisha deni la Ulaya kupitia hati z...
- 
wabunge wa upinzani wakiwa wamesimama wote kwa pamoja kupinga hoja leo Bungeni. Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Up...
- 
Joshua Nassari wapili kushoto . HOJA BINAFSI JUU YA MWENENDO WA BARAZA LA MITIHANI LA TAIFA UNAVYOATHIRI ELIMU YA TANZANIA -...
- 
Mheshimiwa James Mbatia Baada ya hoja binafsi za wabunge wa upinzani `kuzimwa’ bungeni, sasa wanaelekea kutaka kuungwa mkono kupitia ...
Blog zinazovuma
- 
- 
*Photo Editor Free App Download For Pc*. Canva pro is free for all registered nonprofits. Instantly save and share your artwork on any social networking ...
- 
- 
- 
 
Wanaotembelea
NELSON MANDELA
 
Mwanaharakati na mpigania uhuru na mkombozi wa bara la Afrika
MWALIMU JULIUS K NYERERE
 
Mpigania uhuru mwanaharakati,mkombozi wa kweli,mwenye fikra pevu na mwana falsafa
 
Mitandao ya habari
Sikiliza muziki
Nifahamu
 
- Steven Elias
- Musoma, Mara, Tanzania
- Napenda sana kuongea na watu,mpole,nisiyekuwa na makuu...mpenda haki na mwanaharakati wa kweli..
 
 
 
 
 
