KAMATI ya Uchaguzi Klabu ya Yanga imesema inakerwa na tabia ya Baraza  la Wazee la Yanga kuingilia kati masuala ya uchaguzi na kulitaka kukaa  pembeni na kuipa fursa kamati husika kufanya kazi hiyo.
Sambamba  na kauli hiyo, wagombea watatu wa uchaguzi wa klabu hiyo baadaye mwezi  ujao, wamewekewa pingamizi, huku pia zoezi la usaili likipelekwa mbele  mpaka Juni 22.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, John Mkwawa  alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa, kamati yake ni huru hivyo  haipaswi kuingiliwa na mtu au kikundi chochote.
Mkwawa alisema  kamati yake ina mamlaka ya kumchukulia hatua mtu yeyote atakayekwenda  kinyume na taratibu za uchaguzi ambazo wao ndiyo wenye jukumu la  kusimamia.
Kauli hiyo ya Mkwawa imekuja siku moja baada ya  mwanzoni mwa wiki hii baraza hilo ya Yanga kutishia kumfukuza uanachama   Ahmed Falcon.
Falcon alitishiwa kufukuzwa uanachama kufuatia  uamuzi wake wa kuiwekea pingamizi katiba ya Yanga pamoja na wagombea  wote wa uchaguzi huo.
Katika madai yake, Falcon alisema katiba  inayotumika kwenye uchaguzi huo ni batili kwa vile ina upungufu, jambo  ambalo lilipingwa na wazee.
Lakini kwa upande wake, Mkwawa  aliwataka wale wote waliowawekea pingamizi wagombea kwenye uchaguzi huo  kuwasilisha vithibitisho leo Makao Makuu ya Klabu.
Wagombea waliowekewa pingamizi ni pamoja na mfanyabiashara maarufu nchini, Ally Mayayi na Stanley Kevela.
Aidha, Mkwawa amesema kamati yake imetupilia mbali pingamizi la mwanachama Falcon kwa madai kuwa halina msingi.
Mkwawa  alisema madai ya Falcon hayana mashiko na yameshindwa kuwashawishi  kukubaliana naye kwa vile katiba itakayotumika kwenye uchaguzi huo  inatambulika kisheria.
"Katiba inayotumika ni mwaka 2010,  inatambulika kisheria na imepitishwa na Msajili wa Vyama vya Michezo na  kukubaliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)," alisema Mkwawa.
Ikumbukwe  pia kuwa, baraza hilo la wazee Yanga ndilo lililokuwa chemchem ya  vuguvugu la mageuzi ya kutaka mabadiliko ya uongozi kwenye klabu hiyo.
Wazee  hao walianza kwa kutaka kukabidhiwa timu siku chache kabla ya Yanga  kupambana na Simba katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu, ambao Yanga  walifungwa mabao 5-0.Hata hivyo madai yao yalipingwa na uongozi  wa Yanga chini ya Mwenyekiti Llyod Nchunga na baada ya siku chache  wakaanzisha shinikizo la kutaka mwenyekiti wao kuachia ngazi.
Katika  kutimiza matakwa yao, baraza hilo la wazee liliitisha mkutano wa  wanachama uliofanyika Makao Makuu ya Klabu hiyo lakini bila baraka za  uongozi na kutangaza kumtimua Nchunga.
Hata hivyo, mapinduzi hayo  yalipingwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kabla ya Mwenyekiti  Nchunga kukubalia kuachia ngazi baada ya shinikizo la kumtaka kuachia  ngazi kukolea.
Kuhusu
Chat nami hapa
Zinazosomwa sana
- 
Bi:Angela Merkel Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amekataa shinikizo la kujumuisha deni la Ulaya kupitia hati z...
- 
wabunge wa upinzani wakiwa wamesimama wote kwa pamoja kupinga hoja leo Bungeni. Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Up...
- 
Joshua Nassari wapili kushoto . HOJA BINAFSI JUU YA MWENENDO WA BARAZA LA MITIHANI LA TAIFA UNAVYOATHIRI ELIMU YA TANZANIA -...
- 
Mheshimiwa James Mbatia Baada ya hoja binafsi za wabunge wa upinzani `kuzimwa’ bungeni, sasa wanaelekea kutaka kuungwa mkono kupitia ...
Blog zinazovuma
- 
- 
*Photo Editor Free App Download For Pc*. Canva pro is free for all registered nonprofits. Instantly save and share your artwork on any social networking ...
- 
- 
- 
 
Wanaotembelea
NELSON MANDELA
 
Mwanaharakati na mpigania uhuru na mkombozi wa bara la Afrika
MWALIMU JULIUS K NYERERE
 
Mpigania uhuru mwanaharakati,mkombozi wa kweli,mwenye fikra pevu na mwana falsafa
 
Mitandao ya habari
Sikiliza muziki
Nifahamu
 
- Steven Elias
- Musoma, Mara, Tanzania
- Napenda sana kuongea na watu,mpole,nisiyekuwa na makuu...mpenda haki na mwanaharakati wa kweli..
 

 
 
 
 
