Mheshimiwa James Mbatia 
 Baada ya hoja binafsi za wabunge wa upinzani `kuzimwa’ bungeni, sasa wanaelekea kutaka kuungwa mkono kupitia nguvu ya umma.
Wabunge hao wakiongozwa na uratibu wa Chama cha Demokrasia na 
Maendeleo (Chadema), watarejea jijini Dar es Salaam kesho na kupata 
mapokezi, kisha kuandamana hadi wilayani Temeke ambapo watahutubia 
mkutano wa hadhara.
Hata hivyo, Polisi imeonya kwamba mapokezi hayo hayapaswi kuhusisha maandamano, isipokuwa mkutano wa hadhara pekee.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo, alisema 
kinachotarajiwa kufanywa na wapinzani ni mkutano wa hadhara na si 
maandamano.
Lakini Benson alipoulizwa baadaye na NIPASHE Jumamosi, alisema 
chama hicho kimeshaandika barua polisi, kuwataarifu kuhusu maandamano 
hayo.
“Tumewaandikia barua juu ya azma yetu ya kuwapokea wabunge wote wa 
upinzani kesho, kisha maandamano yatakayoanzia Ubungo, Tazara hadi 
Temeke kwenye mkutano wa hadhara,” alisema.
Aliongeza, “maandamano yatakuwa makubwa kwani yatashirikisha vyama vingine vya upinzani ambavyo tumeviandikia barua.” 
Hata hivyo, Kamanda Kiondo, alipotakiwa kutoa ufafanuzi alisema, 
barua ya Chadema imekaa ‘kimtego-mtego’ na kwamba wameibaini ‘janja’ 
yao.
“Maandamano hayatakuwepo, kilichoruhusiwa ni mkutano wa hadhara 
tu,” alisema katika hali inayoashiria (pengine) kukatokea vurugu.
Benson alisema mkutano huo ni mwanzo wa mfululizo wa mikutano 
itakayofanyika kwenye kanda 10 zilizotengwa na Chadema, kuanzia mwenzi 
huu.
“Tunakwenda kuwauliza Watanzania ni Spika na Naibu Spika wa namna gani wanayemtaka,” alisema.
“Huyu Anne Makinda (Spika) na Job Ndugai (Naibu Spika) wamekigeuza 
kiti kile kama kijiwe cha CCM na serikali yao. Kiti wamekigeuza kama cha
 Mungu. Tunataka Bunge ambalo ni sauti ya wananchi na si kijiwe,” 
alidai. 
Aliongeza, “Watanzania ndio watakaoamua kama wanawahitaji Makinda na Ndugai wabaki kwenye nyadhifa zao.” 
Benson alidai kuwa kilichotokea bungeni si kwamba kanuni zina 
matatizo kwa maana zimekuwepo hata wakati wa Bunge lililopita 
likiongozwa na Waziri wa Mambo ya Afrika Mashariki, Samuel Sitta.
Alisema wakati wa Sitta akiwa Spika, Bunge lilikuwa na heshima na 
utaratibu mzuri na hivyo kanuni za sasa `zinaharibiwa’ na Makinda na 
Ndugai.
CUF YAKANA KUSHIRIKI
Wakati Chadema ikisema shughuli hiyo itahusisha vyama vya upinzani,
 Chama Cha Wananchi (CUF) kimejiweka kando na kusema hakitashiriki.
“Hakuna kikao chochote tulichokaa, wanataka kuwahadaa wananchi tu. 
Suala hili ni lao wao wasilazimishe kutushirikisha. Hatutakuwepo,” 
alisema Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro.
Mtatiro alisema inawezekana Chadema wamebaini kuwa Temeke ni ngome 
ya CUF, hivyo wanawahadaa wananchi ili wapate muitikio kwenye maandamano
 na mkutano huo.
“Wakitaka kufanya siasa wafanye tu, lakini wasiwahadae wananchi,” alisema.
Kamanda wa Kanda maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alikana kupata taarifa kuhusu maandamano na mkutano huo.
“Wanawapokea wabunge wao wanatoka Ulaya? Mi sina taarifa hebu wasiliana na kamanda wa Temeke,” alisema.
Kwa upande wake, Kamanda Kiondo alisema,  “taratibu za kuomba 
maandamano zinaeleweka, barua waliyotuletea imeandikwa kimtego-mtego, 
tumewakubalia mkutano na si maandamano.”
Aliongeza, “hawa watu hawana maslahi na hii nchi, wanataka kuleta vurugu tu, kuwatia hasara watu na hata kusababisha mauaji.
“Juzi tu matatizo yametokea Mtwara, leo wanataka kuhamishia Temeke,
 hatukubali. Suala la Dodoma limekwisha jadiliwa limekwisha, hao wabunge
 wao watashuka Tazara watawapokea bila maandamano,” alisema.
Chadema imelazimika kuratibu maandamano hayo na mkutano wa hadhara 
kama ishara ya kumpokea mbunge wao wa jimbo la Ubungo, John Mnyika kwa 
madai ya kufanyiwa mizengwe bungeni kwa kuondolewa kwa hoja yake 
binafsi.
Hoja binafsi ya Mnyika ilikuwa ni kupendekeza Bunge lijadili na 
kupitisha maazimio ya hatua za haraka za kuboresha upatikanaji wa maji 
safi na ushughulikiaji wa maji taka katika jiji la Dar es Salaam, hoja 
ambayo ilitupiliwa mbali na kuzua mtafaruku bungeni.
Hoja nyingine ni ya Mbunge wa Kuteuliwa na Rais, ambaye pia ni 
mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia aliyoitoa bungeni juu ya 
udhaifu wa mitaala ya elimu nchini.
Pamoja na katazo hilo la polisi kuhusu kutokuwepo kwa maandamano 
hayo, lakini maandalizi yalipamba moto huku magari yenye vipaza sauti 
yakiwa yameandaliwa katika ofisi za makao makuu ya Chadema, Kinondoni 
ili  kuwahamasisha watu kujitokeza kwenye maandamano hayo ya kuwapokea 
wabunge wao.
					CHANZO:
					NIPASHE
				
 

 
 
 
 
 
 
 
 
 

After I initially left a comment I appear to have clicked the
ReplyDelete-Notify me when new comments are added- checkbox and from now on each time a comment is added I get four emails
with the exact same comment. Is there a way you are able to remove me from that service?
Thanks!
Also visit my web-site :: Psn Code Generator
I think this is one of the most vital info for me.
ReplyDeleteAnd i'm glad reading your article. But want to remark on some general things, The website style is great, the articles is really excellent : D. Good job, cheers
Also visit my web page ... Dragon city cheat engine