Friday, October 4, 2013

Silvio Berlusconi: Mwisho wa enzi?


Akiwa ametelekezwa na wasaidizi wake, huku akiandamwa na kesi za kisheria, kushindwa kwa Silvio Berlusconi na waziri mkuu wa Italia, Enrico Letta, kunaelezwa kuwa miwsho wake kisiasa.
Waziri mkuu wa zamani wa Italia, Silvio Berlusconi. Waziri mkuu wa zamani wa Italia, Silvio Berlusconi.

"Nadhani tunashuhudia ukurasa wa mwisho katika maisha ya kisiasa ya Berlusconi," alisema Giacomo Marramao, Profesa katika Chuo Kikuu cha Tre cha mjini Roma, baada ya kumalizika kwa kura ya imani kwa serikali katika bunge la Italia. Marramao alisema matokeo ya kura hiyo yaliashiria kupungua kwa kuaminika, akielezea mgawiko miongoni mwa wabunge wa chama cha Berlusconi cha People of Freedom PDL. Profesa huyo alisema chama cha baada ya Berlusconi kimezaliwa siku hiyo ya Jumatano.
Baada ya miongo miwili katika siasa, tajiri huyo machachari ambaye aliwahi kujilinganisha na Yesu, alionekana kubaki mpweke, baada ya makada wake kuanza kumtupa mkono mmoja baada ya mwingine, na kuiunga mkono serikali. Wakati Berlusconi anaondoka bungeni, baada ya kubadili ghafla msimamo wake wa kuiangusha serikali ya waziri mkuu Letta, na kuunga mkono kura ya imani, kundi la waandamanaji lilikuwa nje likimzomea na kumuambia, "Toka hapa."
  Waziri mkuu wa sasa wa Italia, Enrico Letta.
 
Katika kivuli cha Berlusconi halisi
Hata kabla ya kubadili msimamo wake, wachambuzi walisema taarifa zake za kuchanganya zilikuwa zinaonyesha mtu aliyeishiwa nguvu. Stefano Folli, mwandishi wa makala katika gazeti la biashara la kila siku la II Sole 24 Ore alisema Berlusconi alionekana kama kivuli cha Berlusconi wa zamani. Filippo Ceccarelli, mwandishi wa gazeti linaloegemea mrengo wa shoto la La Repubblica, yeye alikwenda mbali na kuilinganisha kura ya Jumatano na Julai 25 mwaka 1943, wakati alipoangushwa rasmi dikteta Benito Mussolini katika kura na baraza kuu la Kifashisti. "Dunia nzima inaanguka," alisema Ceccarelli.

Kitisho halisi kwa Berlusconi hata hivyo, hakitokani na kudhalilishwa kwake bungeni, ambako amefanikiwa kurudi hapo kabla, lakini katika masaibu yake ya kisheria yanayozidi, walisema wachambuzi. James Walston, Profesa wa ushirikiano wa kimataifa katika chuo kikuu cha Marekani mjini Roma, alisema Berlusconi hana tena udhibiti kamili wa chama chake, lakini bado ana nguvu. Lakini aliongeza kuwa masaibu yake ya kisheria yanayoongezeka kila kukicha, yanaashiria kuondoka kwake muda wowote.
Mlolongo wa kesi dhidi yake
Berlusconi anatarajiwa kufukuzwa bungeni mwezi huu, na kuzuwiwa kugombea katika uchaguzi ujao, baada ya kukutikana na hatia katika kesi ya udanganyifu wa kodi mwezi Agosti. Na jaji mjini Milan ataamua mwezi huu, iwapo hukumu ya kifungo cha miezi 12 aliyopewa aitumikie katika kifungo cha nyumbani au afanye kazi za kijamii - hatma ya kufedhehesha kwa bilionea huyo aliyekuwa na nguvu kubwa.

Mambo bado! Ushawishi wa Berlusconi katika siasa za Italia waanza kuyeyuka.
Mambo bado! Ushawishi wa Berlusconi katika siasa za Italia waanza kuyeyuka.
Berlusconi mwenye umri wa miaka 77 pia alikataa rufaa dhidi ya kifungo cha miaka saba jela, alichohukumiwa kwa kufanya ngono na changudoa aliekuwa chini ya umri, na kwa matumizi mabaya ya ofisi alipokuwa waziri mkuu, na vile vile hukumu nyingine ya kifungo cha mwaka moja jela kwa kuvujisha siri za polisi kwa lengo la kumchafua mpinzani wake.
Ishara ya kuanguka kwa Berlusconi ilionyeshwa katika picha zilizosambazwa mapema wiki hii, zikimuonyesha akiwa amebeba mbwa wake katika makaazi yake, katika kile gazeti la La Repubblica lilichosema ni kutokana na ukweli kwamba, mbwa huyo ndiyo kiumbe pekee ambaye kiongozi huyo alieko katika kingo za kuporomoka, anaweza kumuamini.
Lakini Berlusconi amefanikiwa kurudi ulingoni huko nyuma, ingawa hakuwa katika hali ya udhaifu aliyomo hivi sasa, na baadhi ya wachambuzi wameondoa uwezekano wa yeye kutoka katika hili.
Mwandishi: Iddi Ismail Ssessanga/afpe.
Mhariri: Josephat Nyiro Charo.

Warioba awa mbogo


  Amtaka kigogo wa CCM aseme kama ametumwa kuichafua tume
  Asisitiza amemsikia sana akiendesha kampeni ya kuchafua Tume
  1. Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji mstaafu Joseph Warioba
  2. Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji mstaafu Joseph Warioba, amegeuka mbogo na kumtaka Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo, kuacha kupiga kelele dhidi yake kwa kuwa hakumtuma kazi ya kukusanya maoni ya katiba mpya, bali alitumwa na serikali kwa niaba ya wananchi.
    Jaji Warioba alitoa kauli hiyo jana kama karipio kwa Bulembo hilo jijini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, na kusisitiza kwamba Bulembo amekuwa na ajenda ya siri dhidi yake (Warioba) na baadhi ya wajumbe wa Tume kwa kuwa amekuwa akiwazungumzia wao binafsi kila anaposisimama katika majukwaa ya kisiasa.

    Alimtaka Bulembo kuthibitisha kuhusu kauli ambazo amekuwa akizitoa kwenye mikutano ya CCM katika mikoa ya Arusha, Tanga na Mbeya kuwa yeye (Warioba) amegeuka kuwa msemaji wa wananchi katika mchakato mzima wa kupata Katiba mpya.

    Jaji Warioba alitamtahadharisha Bulembo na kumtaka kuacha kupiga kelele pamoja na  kumshambulia badala yake azungumzie masuala yanayohusu Rasimu ya Katiba na siyo kuwajadili wajumbe.

    Aidha, Jaji Warioba alimtaka Bulembo kuthibitisha kama kauli ambazo alizitoa kwa nyakati tofauti katika mikoa hiyo ametumwa na CCM ama ni kauli zake binafsi.

    Jaji Warioba alisisitiza kuwa siku zote Tume yake imekuwa ikitekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria na kuwataka wanasiasa akiwamo Bulembo kujadili Rasimu iliyotolewa badala ya Tume au wajumbe wake.

    Kwa mujibu wa Jaji Warioba, hakutumwa na CCM kufanya kazi anayoifanya na kwamba kazi hiyo alipewa na serikali kwa mujibu wa sheria na kwamba ataendelea kuifanya bila kusikiliza maneno yanayosemwa dhidi yake.

    Alikiri kuwa kauli ambazo zimekuwa zikitolewa na Bulembo kwa nyakati mbalimbali zimechangia mchakato wa Katiba kuwa mgumu hususani wakati wananchi walipokuwa wakitoa maoni kupitia mabaraza ya katiba mkoani Mbeya.

    “Moja ya kazi za kisheria za Tume ni kutoa elimu kwa umma, na ni kazi ya wakati wote.  Sasa kama Bulembo anaona kutoa elimu ni dhambi ni sawa,” alisema Jaji Warioba  ambaye amewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais.

    Kuhusu kukatishwa tamaa kutokana na kauli za wanasiasa hususani kutoka CCM ambao wamekuwa wakimuandama binafsi, Jaji Warioba alisema haogopi wala hatetereki kwa kuwa anafanya kazi aliyotumwa na wananchi.

    Alisema CCM iliishawasilisha maoni yake walipopewa nafasi ya kufanya hivyo, na kwamba masuala mengine yanayojitokeza zikiwamo kauli za Bulembo baada ya hapo hajui zinatoka wapi.

    Aliongeza kuwa Tume yake imekuwa ikifanya kazi katika mazingira magumu kutokana na kauli za wanasiasa mbalimbali na kuongeza kuwa pamoja na kauli hizo, inafarijika na kauli za kutia moyo wanazozipata kutoka kwa wananchi wa kawaida.

    “Nilisema mwishoni mwa mwezi uliopita, wanasiasa wamekuwa wakitoa matamshi yaliyoifanya kazi ya Tume kuwa ngumu katika mikutano ya mabaraza ya katiba,” alisema na kuongeza:

    “Matamshi mengine yalilenga Tume na wakati mwingine yalinilenga mimi binafsi au wajumbe wa Tume badala ya kuzungumzia rasimu,” alisema
    Warioba alisema siku zote Tume yake imekubali kukosolewa kwa kuamini kuwa kukosolewa ni jambo la kawaida, lakini alisisitiza kuwa ni vyema wananchi na wanasiasa wakajadili Rasimu ya Katiba iliyotolewa badala ya watu au Tume.

    “Nadhani wangezungumzia Rasimu wangetusaidia sana, badala ya kuzungumzia Tume na watu,” aliongeza.
    Juzi CCM iliendeleza kauli zake zinazoonyesha kumuingilia na kumshambulia vikali Jaji Warioba na kumtaka aache kuwasemea Watanzania juu ya aina ya Katiba wanayoitaka.

    Matamshi ya kumshambulia Jaji Warioba yalitolewa mkoani Tanga na Bulembo, wakati akihutubia moja ya mikutano ya hadhara ya wanachama wa chama hicho.

    Bulembo alinukuliwa katika vyombo vya habari akisema kuwa siyo sahihi kwa Jaji Warioba kuwa msemaji wa Watanzania kuhusiana na mambo wanayoyataka yaingizwe ndani ya katiba.

    “Jaji Warioba ni mmoja kati ya Watanzania mamilioni na kwa hali hiyo hawezi kubeba mawazo ya Watanzania wengine, ni vizuri akasimamia Rasimu, badala ya kuwa msemaji wa wananchi,” alisema Bulembo ambaye pia ni Mjumbe wa kamati Kuu (CC) ya CCM.

    Kauli hiyo ya Bulembo imetolewa wakati kukiwa na msuguano kati ya CCM na serikali yake kwa upande mmoja, na vyama vitatu vya upinzani vyenye wabunge ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

    Mwishoni mwa mwezi uliopita, Jaji Warioba akizungumza na waandishi wa habari, aliwakemea baadhi ya viongozi wa kisiasa kwa kuiingilia mchakato wa kupata Katiba mpya unaoendelea.

    Alisema baadhi ya changamoto zilizojitokeza wakati wa kuendesha Mabaraza ya Katiba, ni kwa baadhi ya vyama vya siasa kuingilia uhuru wa wajumbe katika kutoa maoni kuhusu Rasimu ya Katiba, wakiwafundisha nini cha kusema.

    Jaji Warioba aliwasihi viongozi wa vyama vya siasa kuwaachia wananchi, cha kusema kwani, katiba inayotafutwa ni ya wananchi, na si ya vyama au kundi fulani

    Bulembo alipotafutwa jana kufafanua kama kauli hizo ni zake binafsi au ametumwa na CCM,hakupatikana kutokana na simu yake ya mkononi kuita bila majibu.
  3. Hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno (sms),pia hakujibu hadi tunakwenda mitamboni
     
CHANZO: NIPASHE

Sunday, May 26, 2013

Sakata La Gesi Mtwara: Tuache Woga, Tuchambue Mchele na Pumba


Taifa letu lipo katika wakati mgumu sana ambao unahitaji maamuzi sio tu MAGUMU lakini pia MAKINI; Lakini Ugumu na Umakini huu Kimaamuzi hatuna budi kuufanya kwa kushirikiana na wananchi wa Kusini badala ya kuwabeza, lakini hasa kuingiza siasa kuliko mantiki katika kulitazama suala zima. Vinginevyo suala la ‘Resource Curse’ ambalo kwa miaka mingi tumekuwa tunalisikia tu kwa wenzetu, sasa litatukuta muda sio mrefu na wahanga watakuwa ni kila mtanzania bila ya kujalisha cheo au uwezo wa fedha; Mengi yameshajadiliwa na wadau mbalimbali kuhusiana na mgogoro huu pamoja na mapendekezo juu ya nini kifanyike ili kuokoa taifa letu lisitumbukie katika janga la ‘resource curse’; Muhimu hapa ni kuwaweka wananchi wa Kusini at the ‘Centre’ katika suala zima la gesi asilia na economic development, sio kuwaweka at the ‘Periphery’. Pia ni muhimu serikali ikatambua kwamba wananchi wa kusini wanazidi kuelimishwa kwamba faida kwao itatokana zaidi na ubora wa ‘Natural Gas Policy’, ambayo kwa bahati mbaya, tayari tunaingia katika mikataba mikubwa huku ‘Natural Gas Policy’ ikiwa katika hatua ya ‘Draft Document’; Ni masuala kama haya ndio yanachangia sana kwa serikali ‘to shoot on its own foot, na mbaya zaidi, tiba zinazotatumiwa kutibu jeraha ni tiba ambazo zinazidi kuchimba kidonda kuliko kukikausha. Ni muhimu kwa viongozi wa Serikali sasa kuja na maamuzi magumu na makini ambayo yatalenga kurudisha imani ya wananchi wa mtwara kwa serikali yao; Huu sio wakati wa siasa za ubabe na arrogance, na pia vyama vyote vya siasa ni vyema vikaliondoa suala hili majukwaani na badala yake kutafuta mazingira ya kukaa meza ya pamoja na kulifanya suala hili kuwa ‘bipartisan’ kama kweli nia ni kurudisha hali ya amani na utulivu katika taifa letu;

Leo hii, Tanzania inakadiriwa kuwa na utajiri wa gesi asilia unao karibia
43 trillion cubic feet; Hifadhi hii inakadiriwa kuwa na thamani ya dollar za kimarekani karibia Billion 450, ambayo ni sawa na karibia Shillingi trilioni 730; US geological Survey inakadiria uwepo wa hifadhi kubwa zaidi na kwamba tafiti zinazoendelea zitabainisha uwepo wa gesi wa karibia 441 trillion Cubic feet; Nyingi ya gesi hii inakadiriwa kuwepo katika maeneo ya Pwani ya Afrika mashariki, huku Tanzania ikiwa ni sehemu kubwa ya eneo hilo; Ni kwa maana hii, inakadiriwa kwamba miaka kumi ijayo, Tanzania itakuwa ni moja ya mataifa yanayozalisha gesi asilia kwa wingi Duniani; Na ni kwa mantiki hii ndio maana kampuni mbalimbali za sekta ya gesi duniani kama vile British Gas imejipanga kuwekeza Tanzania Dollar billioni 15 (kumi na tano) sawa na shillingi trilioni 24 (ishirini) na nne kwenye sekta ya gesi nchini katika kipindi cha miaka kumi ijayo; Tufahamu kwamba Dollar Bilioni Kumi na Tani ni zaidi ya nusu ya pato la sasa la nchi (GDP) ya Tanzania!!!

Migogoro yote itokanayo na rasilimali aka ‘natural resource curse’, chanzo chake huwa ni tatizo la
rent-seeking behavior na short terms gains on part of politicians and other public officials;Watanzania wanazidi kuchoka kuishi na ahadi za kisiasa majukwaani wakati wa kampeni za chaguzi kuu mbalimbali; Vinginevyo katika suala la rasilimali kama hizi (gesi), suala la faida kwa wananchi ni suala la common sense, kwani halihitaji rocket science kutambua kwamba ukosefu wa culture of transparency katika mikataba, hasa isiyoshirikisha wadau; Ndani ya dunia ya leo inayosukumwa na nguvu za utandawazi, wananchi hawahitaji kufundishwa na mtu yoyote kutambua kwamba the expected ‘revenues and investments’ from Gas, Oil, or Gold ni lazima zisaidie nchi to shift towards industrialization na kuzalisha ajira, huku pia mapato kupitia kodi yakienda kuboresha miundo mbinu, sekta za afya, elimu, na maji; Na katika haya, ni common sense kwamba wananchi wa kupewa kipaumbele ni wa vijijini, lakini hasa wale ambao wapo nyuma kimaendeleo kulinganisha na wananchi wa mikoa mingine;

Sasa inapotokea kwamba rasilimali husika inatokea maeneo yao lakini hakuna transparency katika mchakato mzima wa utilization ya rasilimali husika, migogoro lazima itajitokeza; Ni kwa mantiki hii, wananchi wa kupewa kipaumbele katika hili ni wananchi wa mikoa ya kusini ambao kwa zaidi ya miaka 50 wamekuwa hawapewi kipaumbele in terms of economic development ikilinganishwa na sehemu nyingine nyingi za nchi; Kwa maana hii, ingawa ni sahihi kusema kwamba Gesi ya Mtwara ni ya Watanzania wote, lakini pia ni sahihi kusema kwamba kwa simple logic tu ya ‘sustainability’ – kisiasa, kiuchumi, kijamii na kimazingira, faida ya gesi hii ni lazima iwe wazi kwanza pale inapotoka (source); Hivi ndivyo mataifa yaliyoendelea yalifanya; Kwa kuzingatia tu ‘simple economics’, mkoa wa Mtwara una mazingira yote muhimu yanayokidhi approach ya namna hii; kwa mfano, Mtwara tayari kuna Bandari, kuna nguvu kazi iliyo ‘idle’ ambayo kutokana na sera mbovu za serikali, nguvu kazi hiyo imegeuka kuwa wachuuzi nchi nzima, pia Mtwara ina eneo kubwa la Ardhi kwa ajili ya maendeleo ya Kilimo na Viwanda; Muhimu zaidi, Mtwara ni a better gateway kwa maendeleo ya uchumi ndani ya SADC Zone; Ni masuala kama haya ndio yanawia vigumu watu wengi kuamini kwamba ni Lazima gesi itokea kwanza Mtwara kwenda sehemu nyingine ya nchi, halafu wananchi wa mtwara waje kupata faida za gesi hii baadae; Hata simple economics zinazozingatia factors nilizojadili hapo juu zinathibitisha kwamba approach ya
is not the best alternative kiuchumi; pengine; it’s the best alternative kisiasa, hasa in the context of rent seeking behavior and short terms gains kwa wahusika;

Ebu tuujadili mkoa wa Mtwara Kidogo


Duniani kote, GDP Per Capita ni kiashiria (indicator) cha hali ya wananchi kiuchumi i.e. kipato/income. Zifuatazo ni takwimu za pato la kila Mtanzania kwa mwaka 2010 - Nimechukua kumi bora na kuziweka in ‘order of ranking’:


Jedwali la Kwanza: Vipato Vya Watanzania Kulingana na Mikoa Wanayotoka (GDP Per Capita)


MKOA PATO LA KILA MWANANCHI KWA MWAKA (T.Shillings) (2010)
1. Dar-es-salaam 1,740,947 (million)
2. Iringa 979,882 (laki)
3. Arusha 945,437
4. Mbeya 892,877
5. Kilimanjaro 879,432
6. Ruvuma 866,191
7. Mwanza 829,647
8. Tanga 763,203
9. Morogoro 744,234
10. Rukwa 726,658
Source: Bajeti Za Serikali.

Tukitizama jedwali namba moja, Mikoa ya Kusini (kama Mtwara) haipo katika orodha hii
; Je, hii ni kwa sababu gani? Pengine tutazidi elewa ndani ya mjadala wetu baadae, lakini kwa sasa tutazame takwimu nyingine:

  • Je, ni Mikoa ipi inachangia Zaidi Kwenye Pato la Taifa/Inayozalisha Bidhaa na Huduma Nyingi Zaidi Tanzania (GDP)?


Jedwali la Pili: Kumi Bora Kwa Uzalishaji Wa Bidhaa na Huduma (GDP).


MKOA UZALISHAJI WA BIDHAA NA HUDUMA (GDP) T.shillings (2010)
1. Dar-es-salaam T.sh 5.4 trillioni
2. Mwanza T.sh 3.0 trillioni
3. Mbeya T.sh 2.3 trillioni
4. Shinyanga T.sh 1.9 trillioni
5. Iringa T.sh 1.7 trillioni
6. Morogoro T.sh 1.6 trillioni
7. Arusha T.sh 1.5 trillioni
8. Kilimanjaro T.sh 1.3 trillioni
9. Kagera T.sh 1.3 trillioni
10. Ruvuma T.sh 1.2 trillioni
11. Tabora T.sh 1.2 trillioni
12. Rukwa T.sh 1.1 trillioni
Source: Bajeti Za Serikali.

Vile vile, tukitazama jedwali la pili hapo juu, mikoa ya kusini (e.g. Mtwara) pia haipo katika kumi bora katika mchango wa uzalishaji na pato la Taifa; Swali linalofuata ambalo ni la kimantiki zaidi hasa kiuchumi kuliko siasa ni je:


  • Kwanini sasa tusitumie fursa hii ya gesi asilia mikoa ya kusini kuigeuza mikoa hii na yenyewe iwe na mchango kwa pato la taifa?


Binafsim nadhani ugunduzi wa gesi ya Asilia ndio fursa pakee iliyopo ya kuifanya mikoa ya kusini nayo iwe na mchango mkubwa kwa pato la taifa kupitia uwekezaji utakaotokana na mapato ya gesi; Nasema kwamba ni fursa pekee kwa sababu kwa miaka zaidi ya hamsini, wananchi wa kusini kama nilivyokwisha jadili, wamekuwa wakipuuzwa kimaendeleo; Inaonekana kwamba sera ya serikali ni kuwekeza katika maeneo yenye michango mikubwa kwa pato la taifa (GDP contribution) na ushahidi katika hili upo kwenye takwimu juu ya vipaumbele vya bajeti kwa mikoa mbalimbali kila mwaka; Ushahidi wa hili upo katika jedwali lifuatalo:


Jedwali la tatu: Mikoa Yenye Michango Midogo Katika Uzalishaji/Pato la Taifa (bottom 5).


MKOA UZALISHAJI WA BIDHAA NA HUDUMA (GDP) T.shillings (2010)
1. Singida T.sh Billioni 661
2. Pwani T.sh Billioni 608
3. Lindi T.sh Billioni 621
4. Kigoma T.sh Billioni 906
5. Mtwara T.sh Billioni 927
Source: Bajeti Za Serikali.

Tukitazama jedwali la tatu, tunaona Mtwara, Lindi na mikoa mingine kwamba ni ya mwisho kabisa katika kuchangia pato la taifa (GDP contribution in terms of production of Goods and Services); N
ote pia Kigoma ni sehemu ya orodhahii na hatupo mbali na mgogoro mwingine mkubwa katika mkoa huu; Vinginevyo si ajabu ndio maana mikoa hii imekuwa ikitengewa fedha ndogo katika bajeti za kila mwaka kama tunavyoona kwenye jedwali namba nne hapo chini:

Jedwali la nne: Mikoa inayotengewa fedha ndogo za Bajeti (bottom five)


MKOA BAJETI YA MWAKA (T.sh) (2010)
1. Mtwara T.sh Billioni 57
2. Kigoma T.sh Billioni 56
3. Singida T.sh Billioni 50
4. Manyara T.sh Billioni 54
5. Rukwa T.sh Billioni 49
Source: Bajeti Za Serikali

Je ni mikoa gani ambayo inapewa kipaumbele katika kila bajeti? Jibu ni – Mikoa ile ile ambayo ndio inachangia kwa kiasi kikubwa pato la taifa (GDP) kama ambavyo tuliona katika jedwali namba mbili hapo juu; Mikoa hiyo pamoja na kiasi cha fedha wanazotengewa katika bajeti ni kama ifuatavyo:


Jedwali la tano: Orodha ya kumi bora – vipaumbele katika Bajeti Ya Serikali.


MKOA BAJETI YA MWAKA (T.sh)
1. Dar-es-salaam T.sh Billioni 154
2. Mwanza T.sh Billioni 135
3. Mbeya T.sh Billioni 109
4. Shinyanga T.sh Billioni 104
5. Kilimanjaro T.sh Billioni 100
6. Tanga T.sh Billioni 92
7. Kagera T.sh Billioni 88
8. Morogoro T.sh Billioni 86
9. Iringa T.sh Billioni 85
10. Arusha T.sh Billioni 81
Source: Bajeti Za Serikali


Hitimisho


Njia pekee ya ya serikali kutegua bomu lililopo ambalo linaweza pelekea nchi yetu kuingia katika machafuko yasiyokuwa ya lazima ni kwa kuzingatia hoja nilizojenga huko juu; Nimeelezea kwa hoja na takwimu juu ya jinsi gani mikoa mingi ikiwepo ya kusini mwa Tanzania imekuwa ikipuuzwa kimaendeleo kwa miaka zaidi ya hamsini kutokana na sababu moja tu kubwa -
Kutokuwa na mchango wa maana kwa pato la taifa; Kama nilivyobainisha kwa hoja na takwimu, mikoa inayopewa kipaumbele katika bajeti zetu ni ile inayochangia zaidi katika pato la taifa (GDP); Kwa mantiki hii, ni muhimu kwa Serikali kusikiliza vilio vya wananchi wa kusini ili na wao wawe sehemu ya mikoa iliyopo katika jedwali namba tano hapo juu; Vinginevyo, kama nilivyokwisha sema awali, the government is shooting on its own foot, na mbaya zaidi, its prescribing tiba ambayo sio sahihi, huku kidonda kikizidi kuchimbika; Sidhani kama serikali ina nia ya kuendelea kuzembea katika hili na kupelekea mguu kukatwa na madaktari kama njia pekee itakayobakia kutibu tatizo;

Monday, April 15, 2013

Mwigulu nae anapaswa kuhojiwa Mahakamani,



Mwigulu Mchemba Naibu Katibu CCM Bara,
Mbunge Jamhuri ya Muungano Tanzania


Mwigulu Mchemba mhusika mkuu Movie ya Rwekatare
Mwigulu Mchemba Mhusika Mkuu katika kashfa ya filamu inayodaiwa kuwa ya ugaidi ambaye amejipambanua na kutangaza hadharani kupitia:
  1. Chombo cha habari TV Desemba Mwakajana
  2. Mtandao wa Jamii Forums kiambatanisho cha nukuru JF hapo chini Jana tarehe 29/03/2013 hapo chini

Ameandika kwamba alikabidhiwa mkanda huo na mmoja wa viongozi wa Chadema, akiwa ni verified user member wa JF Mwigulu Mchemba amekiri kuhusika na mkanda huo, polisi kwa kutumia weledi unaotakiwa kisheria Mwigulu Mchemba ashikwe na kuunganishwa katika kesi hiyo kwani ndiye mwenye kuleta jawabu kamili namna alivyoupata mkanda huo, aliyempa na makandokando yake.

Kinyume cha kutofanya hivyo ni ushahidi movie hiyo kutengenezwa kwa ushirikiano wa huyu Mwigulu Mchemba na vyombo vya usalama ndio maana analindwa kutohusishwa katika kesi hii ingawa kuna ushahidi wa wazi kuhusika.

NB:
Hata vyombo vya dola vikiendelea kumkwepesha kwa kumlinda, taratibu na sheria za mahakama hatakwepa kuunganishwa katika kashfa hiyo kwani anaonekana ndiye shahidi maalum katika kesi hiyo kwa vile hajaonyesha siri kwani amejipambanua muda mrefu wa kutosha kuhusika na movie hii.


Mwigulu Nchemba


By king kan
Kama umejifunza uzalendo na utiifu kwa taifa. Prove your words by doing yafuatayo: 1. Saidia kueleza watanzania na polisi juu ya mkanda wa mauaji katika nyanja zifuatazo wewe uliupataje, nani alikupatia hiyo kopi na kwa nini hukutoa taarifa kwa vyombo vya dola na badala yake ulitumia media? 2. Uhalali wa elimu yako na jina lako ili tujue kama hukuiba fursa ya mtanzania mwingine ya kupata elimu? Kwa sasa nijibu kwanza hayo.

By Mwigulu Mchemba
King Swala liko mahakamani kumtaja aliyenipa itahatarisha maisha yake ila ni kiongozi wa chadema. Kuhusu elimu na jina mimi nilisoma mpaka darasa la tano nikaacha nikaenda kambini kuchunga mifugo nikarudi shule after 2 year nimefanya mtihani wa darasa la saba mwenyewe sijampoka mtu nafasi. Jina linawachanganya bure nilipewa la nesi aliyenipokea baada ya kuzaliwa home. Ndiye alikuwa akiitwa Mwigulu/Lameck. Mimi nilikuwa nikiitwa Mugulo. Mkanda nilipeleka vyombo vya usalama kabla ya media ila wao wananamna ya kuchunguza

Update

Kauli ya Tundu Lissu

Ukiacha sakata hilo ndani ya Chadema, Mnidhamu wa chama hicho, Tundu Lissu, yeye hataki kuuma maneno na hivyo ameamua kupasua jipu. Amesema ushahidi uliopatikana unaeleza kuwa siku chache baada ya kurekodi mkanda huo,
Mwigulu Nchemba alimtumia Ludovick Sh 50,000 kupitia mtandao wa Vodacom, hivyo anahoji zilikuwa za nini.
“Hivi leo Sh 50,000, si milioni Sh 5,000,000 au kumi ni Sh 50,000 tu zinasababisha amsaliti mtu wake wa karibu na kumsabishia alale Magereza?

Ludovick aisaliti familia iliyomsaidia
Lissu anasema anashangaa kusikia Ludovick ameamua kuisaliti familia ya Lwakatare kwa kuwa alikuwa ni mtu wa karibu wa familia hiyo, kwani Lwakatare na mkewe ndiyo waliosimamia na kufanikisha ndoa ya Ludovick. Amesema Ludovick pia ndiye aliyekuwa wakala wa Lwakatare katika kusimamia kuhesabu kura wakati akigombea ubunge mwaka 2010 jimboni Bukoba. Hata hivyo, Lissu anakiri kuwa Ludovick alikuwa mwanachama mtiifu wa Chadema na alikuwa katika kikosi cha Blue Guard, ila anahoji:
“Ninavyoijua afya ya Lwakatare ilivyo, asipokula tu inakuwa mgogoro unafikiri kesho Ludovick ataonekana vipi kwa watoto wa Lwakatare,” amesema. Lissu amesema kupitia mkakati aliouita wa ‘kishamba’, kamwe Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakitaiangusha Chadema bali ni kuzidi kukipa umaarufu siku za usoni.

Ludovick alivyorekodi mkanda
Amesema Desemba 28 mwaka jana saa 5 asubuhi Ludovick alikwenda nyumbani kwa Lwakatale na saa 5:59 na
akiwa hapo alimpigia simu Nchemba kwa namba iliyoorodheshwa kwenye kitabu cha Bunge kutaarifu kuwa amefika. Ameongeza kuwa kwa kuwa Ludovick alikuwa kama mtoto wa nyumbani, aliingia nyumbani kwa Lwakatare muda wowote na kukaa sehemu yeyote, hivyo siku hiyo ndiyo aliyoamua kufanya kazi hiyo kwa kumuliza Lwakatare maswali ya mtengo.

Amesema katika mkanda huo inasikika sauti ya Ludovick ikiuliza maswali ambayo yanatengeneza jibu, ambayo hutumika kama mtego wa kumtega muulizwaji ili atoe jibu analotaka muulizaji. Lissu amesema, hata hivyo, anashukuru majibu yaliyotolewa na Lwakatare hayakuwa kama muulizaji alivyotaka. Amesema kuwa iwapo angejibu kama Ludovick alivyotaka Chadema ingekuwa na hali mbaya na kesi hiyo ingekuwa ngumu kwao.

Historia ya Ludovick utata
Wakati mahakama ikisubiriwa kusikiliza na kutoa uamuzi wa mashitaka yaliyofunguliwa dhidi ya watuhumiwa, habari zilizopatikana zinasema Ludovick amekuwa akiishi maisha ya “aina yake”.


  • Habari za uhakika zinasema kwamba mtuhumiwa huyo amepata kupewa hifadhi katika familia moja mjini Morogoro, baada ya kujitambulisha kuwa ni yatima. Kwa maelezo yake, aliomba msaada wa kusomeshwa, na akafanikiwa kupelekwa katika Chuo cha Ualimu Morogoro.
  • Imeelezwa kwamba katika kipindi hicho, alifahamiana na mtu mmoja mwenye asili ya Mkoa wa Mara (jina tunalo), ambaye alimwezesha kupata hifadhi nyumbani kwa mmoja wa viongozi katika mhimili mmoja hapa nchini (jina tunalihifadhi kwa sasa).
  • Hapo alieleza kwamba alikwama kusoma seminari kutokana na kufiwa na wazazi. Imeelezwa kwamba, akiwa nyumbani kwa msamaria mwema huyo, siku moja, usiku wa manane, aliruka ukuta na kutokomea, lakini aliweza kurejea saa 9:30 usiku.
  • “Baada ya kutoka tulimweleza bosi wetu, akaamua tukae nje tusubiri tuone kama atarudi. Kweli, alirudi 9:30 usiku, ajabu ni kwamba ukuta ulikuwa mrefu sana, lakini aliweza kuruka kwa namna ambayo sote tulishangaa.“Bosi wetu kuona hivyo akaamua kumfukuza. Lakini kabla ya hapo alimhoji na yeye akasema hajui namna anavyoweza kuruka ukuta, akasema ana matatizo ya akili,” amesema mmoja wa walinzi.
  • Habari nyingine zimesema kwamba akiwa Morogoro aliweza kuongoza ibada kadhaa za mazishi za madhehebu Katoliki. “Hatukumsikia tena baada ya kutoka Morogoro hadi tulipopata taarifa kwamba anasoma DUCE jijini Dar es Salaam,” kimesema chanzo chetu.


Update
Mwigulu akiri kuhusika video ya Lwakatare

  • HATIMAYE Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Mwigulu Nchemba, amekiri kuhusika na video inayomwonesha Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare.

Nchemba amekuwa akitajwa na viongozi wa CHADEMA kuwa anahusika kutengeneza video hiyo, kwa kuwa aliwahi kutamba wakati akihojiwa na kituo kimoja cha televisheni kuwa anayo video inayowaonesha viongozi wa chama hicho wakipanga mauaji.

Hata hivyo, tangu Nchemba atoe kauli hiyo Januari mwaka huu, Jeshi la Polisi lilikaa kimya hadi Machi 12 lilipomkamata na kumhoji Lwakatare, siku moja baada ya video hiyo kuwekwa kwenye mtandao wa You tube na mtu anayejiita ‘Bukoba Boy’.


Akizungumza na gazeti hili kwa simu jana, Nchemba alikiri kuwa ndiye aliyeipeleka video ya Lwakatare polisi na kwamba alifanya hivyo baada ya kuripoti kuandikiwa ujumbe wa simu wa kutishiwa maisha na baadhi ya viongozi wa CHADEMA.
“Niliwapelekea mimi hiyo video polisi na wakati nasema kwenye televisheni nilikuwa tayari nimewapa. Na pale nilisema makusudi baada ya Zitto Kabwe kudai kuwa mwaka jana kulitokea mauaji mengi, ndipo nikataka kumuonesha kuwa chama chake kinahusika na mikakati hiyo,” alisema.


Alipoulizwa aliipataje video hiyo na kwanini hajahojiwa polisi ili kutoa uthibitisho wa uhalali wake, Nchemba alisema: “Kuna msamaria mwema aliniletea.”
Nchemba alipobanwa ana uhakika gani kama video hiyo ina ukweli, alijibu kuwa: “Ile huhitaji akili kubwa kutambua uhalisia wake. Suala la Lwakatare CHADEMA wakubali tu na wajitokeze hadharani kwenye makanisa na misikiti, watubu na kuomba radhi kwa umma.”


Mchemba atoa siri za mahojiano Polisi na Rwekatare
Hata hivyo katika kile kinachoweza kuongeza mashaka ya Nchemba kuhusishwa kutengeneza video hiyo, alikwenda mbali zaidi akitoa hata siri za polisi, akisimulia maelezo aliyodai kuwa ndiyo yalitolewa na Lwakatare wakati akihojiwa na polisi.
“Pale video inaonesha ni nyumbani kwake, tena jikoni na hilo amekiri katika maelezo yake polisi. Pia amekubali kuwa siku hiyo alipiga chafya kama inavyoonekana. Sasa wewe mwandishi unatetea nini wakati yeye amekiri polisi kila kitu kilichomo mle,” alisema.

Maelezo ya Nchemba yalionekana kumtia hofu mmoja wa mawakili wa Lwakatare, ambaye alikuwepo wakati wote wa mahojiano polisi, Nyaronyo Kicheere, akidai kuwa ni wazi jeshi hilo linafanya kazi ya propaganda za CCM.
“Nchemba hakuwepo wakati Lwakatare akihojiwa na hata baadhi ya wanasheria katika kesi yake ya ugaidi inayomkabili hawajui alichokisema polisi, sasa huyo amepata wapi siri za polisi kama si mchezo unachezwa?” alihoji.

Kuhusu mahusiano yake na mshtakiwa wa pili katika kesi ya Lwakatare, Ludovick Joseph, ambaye anadaiwa na baadhi ya watu kuwa ndiye aliyerekodi video hiyo, Nchemba alisema walifahamiana kupitia mtandao wa kijamii wa facebook.
Alipotakiwa kufafanua ukaribu wao hadi kufikia hatua ya kumtumia fedha kwa njia ya M-Pesa kupitia simu yake, Nchemba alisema: “Mimi nilimtumia kama ninavyowapa watu wengine hata wa CHADEMA. “Mimi sijui kama Ludovick ndiye alirekodi video hiyo, wala sikuwahi kumtuma kufanya hivyo na fedha niliyomtumia si kwamba nilikuwa nikimlipa ujira. Kwani unaweza kumpa mtu sh 50,000 tu kwa kazi hiyo?” alihoji.


Tanzania Daima lilipotaka kufahamu kama anahusika kushirikiana na vyombo vya dola kuwarubuni baadhi ya vijana wa Makao Makuu CHADEMA kwa fedha ili watumike kutoa ushahidi wa kumwangamiza Lwakatare mahakamani, Nchemba alisema: “CHADEMA haijawahi kuongoza serikali, hivyo hawajui mikono ya serikali.”


Alipotakiwa kufafanua kikao baina yake na vijana hao kilichofanyika katika Hoteli ya Sea Cliff ya jijini Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi uliopita na kisha kuwatumia fedha kwa njia ya M-Pesa, Nchemba aling’aka na kuuliza: “Hiyo Hoteli ya Sea Cliff iko wapi? Maana sipajui na sijawahi kufika.”
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Mkurugenzi wa Mambo ya Katiba wa CHADEMA, Tundu Lissu, alifichua njama zinazofanywa ili kutengeneza ushahidi wa uongo kwa ajili ya kuutumia katika kesi ya ugaidi inayomkabili Wilfred Lwakatare.


Lissu alidai kuwa njama hizo zinafanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama na ujasusi ili kutumia ushahidi huo mahakamani dhidi ya Lwakatare.
Alisema kuna baadhi ya vijana wa CHADEMA wa Idara ya Ulinzi na Usalama wanaopewa fedha na kuahidiwa kufundishwa namna ya kuzungumza katika kesi hiyo ya Lwakatare. Lissu alisema kuna baadhi ya vijana wakiongozwa na Saumu Mulugu, ambaye alifukuzwa kazi CHADEMA mwanzoni mwa mwaka jana, wamepokea fedha kutoka kwa kigogo mmoja wa CCM (jina linahifadhiwa) ili kufanikisha mpango huo.


Lissu alisema hadi sasa vijana hao wameshapewa sh 400,000 ili wakubali kwenda kufundishwa jinsi ya kuzungumza mahakamani kuwa CHADEMA ni chama cha kigaidi, kwamba Lwakatare alipanga mikakati ya kigaidi.
“Awali walipewa sh 400,000, wakapewa tena sh 300,000, pia wakapewa sh 35,000 mara mbili. Na fedha zote hizi walikuwa wanapewa kwa njia ya M-Pesa,” alisema Lissu. Alidai kuwa Saumu ndiye anayeratibu mpango wote kati ya Jeshi la Polisi na vijana hao wa CHADEMA kwa kuwarubuni kwa fedha.

Alisema vikao baina ya vijana hao wa CHADEMA na Saumu vimewahi kufanyika mara kadhaa katika moja ya hoteli maarufu nchini juu ya mambo ya kwenda kuzungumza kwenye vyombo vya habari au mahakamani kwenye kesi ya Lwakatare.

Tanzania daima yanasa mawasiliano ya Saumu na wenzake
Siku moja baada ya madai ya Lissu, gazeti hili lilimnasa Saumu akiwa anawasiliana na wenzake, huku akiwatuhumu baadhi yao kuwa ndio waliovujisha siri kwa Lissu.
Vilevile alionekana akiwasiliana na kigogo mmoja wa CCM ambaye alikuwa akimwita ‘mkuu’ huku akimsomea baadhi ya taarifa zilizoandikwa magazetini jana yake kuhusu kuvuja kwa siri zao.


Saumu akiwa katika grosari karibu na baa maarufu kwa jina la Kwa Kimaro, jirani na eneo la Benki Kuu ya Damu Salama, Mchikichini jijini Dar es Salaam, alisikika akiwalalamikia wenzake kwa kumsaliti na kuvujisha mkakati wao kwa Lissu.
“Kwanini mmelikisha siri zetu kwa Lissu hadi amejua tulikutana katika hoteli ya kifahari na Mwigu…? Sasa nitawaonesha, maana laki tano zenu ninazo mimi. Siwapi bali nitazitumia kujilinda,” alitamba.


Saumu ambaye alikuwa akizungumza kwa sauti kubwa ya ghadhabu kupitia simu, aling’aka: “Nyie kwanini mmeniuza kwenye ishu ambayo tumeipanga wote?”
Baada ya kupokea maelekezo kutoka kwa ‘mkuu wake’ aliendelea kupiga simu akimlalamikia mtu ambaye hakumtaja, kuwa alikuwa amezima simu yake makusudi kwa kuwa ndiye alivujisha siri zao kwa CHADEMA. “Mimi sitakubali na nimehakikishiwa na bosi wetu kuwa huyo aliyetusaliti tutatumia wale askari kumwekea hata unga. Haiwezekani fedha tumepokea za kwanza, za pili na tatu kwanini tuuzane dakika za mwisho?” alidai Saumu huku akiendelea kugida bia yake.


Huku akihaha huku na kule, Saumu alikuwa akiwapigia simu baadhi ya madereva wa CHADEMA makao makuu na kuwaomba simu za baadhi ya watu, na hata wakati mwingine kuwafokea akidai ndio waliofichua siri hiyo.
Hata hivyo, baada ya kutilia shaka nyendo za chanzo chetu kudaka siri zake, ghafla alitokomea na kuzima simu zake mara moja kwani hata alipotafutwa baadaye hakupatikana hadi leo.

Saturday, February 9, 2013

BAADA YA HOJA ZAO 'KUTUPWA' BUNGENI:Wabunge wa upinzani kutua Dar kwa kishindo

Mheshimiwa James Mbatia
 Baada ya hoja binafsi za wabunge wa upinzani `kuzimwa’ bungeni, sasa wanaelekea kutaka kuungwa mkono kupitia nguvu ya umma.
 
Wabunge hao wakiongozwa na uratibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), watarejea jijini Dar es Salaam kesho na kupata mapokezi, kisha kuandamana hadi wilayani Temeke ambapo watahutubia mkutano wa hadhara.
 
Hata hivyo, Polisi imeonya kwamba mapokezi hayo hayapaswi kuhusisha maandamano, isipokuwa mkutano wa hadhara pekee.
 
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo, alisema kinachotarajiwa kufanywa na wapinzani ni mkutano wa hadhara na si maandamano.
 
Lakini Benson alipoulizwa baadaye na NIPASHE Jumamosi, alisema chama hicho kimeshaandika barua polisi, kuwataarifu kuhusu maandamano hayo.
 
“Tumewaandikia barua juu ya azma yetu ya kuwapokea wabunge wote wa upinzani kesho, kisha maandamano yatakayoanzia Ubungo, Tazara hadi Temeke kwenye mkutano wa hadhara,” alisema.
 
Aliongeza, “maandamano yatakuwa makubwa kwani yatashirikisha vyama vingine vya upinzani ambavyo tumeviandikia barua.” 
 
Hata hivyo, Kamanda Kiondo, alipotakiwa kutoa ufafanuzi alisema, barua ya Chadema imekaa ‘kimtego-mtego’ na kwamba wameibaini ‘janja’ yao.
 
“Maandamano hayatakuwepo, kilichoruhusiwa ni mkutano wa hadhara tu,” alisema katika hali inayoashiria (pengine) kukatokea vurugu.
 
Benson alisema mkutano huo ni mwanzo wa mfululizo wa mikutano itakayofanyika kwenye kanda 10 zilizotengwa na Chadema, kuanzia mwenzi huu.
 
“Tunakwenda kuwauliza Watanzania ni Spika na Naibu Spika wa namna gani wanayemtaka,” alisema.
 
“Huyu Anne Makinda (Spika) na Job Ndugai (Naibu Spika) wamekigeuza kiti kile kama kijiwe cha CCM na serikali yao. Kiti wamekigeuza kama cha Mungu. Tunataka Bunge ambalo ni sauti ya wananchi na si kijiwe,” alidai. 
 
Aliongeza, “Watanzania ndio watakaoamua kama wanawahitaji Makinda na Ndugai wabaki kwenye nyadhifa zao.” 
 
Benson alidai kuwa kilichotokea bungeni si kwamba kanuni zina matatizo kwa maana zimekuwepo hata wakati wa Bunge lililopita likiongozwa na Waziri wa Mambo ya Afrika Mashariki, Samuel Sitta.
 
Alisema wakati wa Sitta akiwa Spika, Bunge lilikuwa na heshima na utaratibu mzuri na hivyo kanuni za sasa `zinaharibiwa’ na Makinda na Ndugai.
 
CUF YAKANA KUSHIRIKI
 
Wakati Chadema ikisema shughuli hiyo itahusisha vyama vya upinzani, Chama Cha Wananchi (CUF) kimejiweka kando na kusema hakitashiriki.
 
“Hakuna kikao chochote tulichokaa, wanataka kuwahadaa wananchi tu. Suala hili ni lao wao wasilazimishe kutushirikisha. Hatutakuwepo,” alisema Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro.
 
Mtatiro alisema inawezekana Chadema wamebaini kuwa Temeke ni ngome ya CUF, hivyo wanawahadaa wananchi ili wapate muitikio kwenye maandamano na mkutano huo.
“Wakitaka kufanya siasa wafanye tu, lakini wasiwahadae wananchi,” alisema.
Kamanda wa Kanda maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alikana kupata taarifa kuhusu maandamano na mkutano huo.
 
“Wanawapokea wabunge wao wanatoka Ulaya? Mi sina taarifa hebu wasiliana na kamanda wa Temeke,” alisema.
 
Kwa upande wake, Kamanda Kiondo alisema,  “taratibu za kuomba maandamano zinaeleweka, barua waliyotuletea imeandikwa kimtego-mtego, tumewakubalia mkutano na si maandamano.”
 
Aliongeza, “hawa watu hawana maslahi na hii nchi, wanataka kuleta vurugu tu, kuwatia hasara watu na hata kusababisha mauaji.
 
“Juzi tu matatizo yametokea Mtwara, leo wanataka kuhamishia Temeke, hatukubali. Suala la Dodoma limekwisha jadiliwa limekwisha, hao wabunge wao watashuka Tazara watawapokea bila maandamano,” alisema.
 
Chadema imelazimika kuratibu maandamano hayo na mkutano wa hadhara kama ishara ya kumpokea mbunge wao wa jimbo la Ubungo, John Mnyika kwa madai ya kufanyiwa mizengwe bungeni kwa kuondolewa kwa hoja yake binafsi.
 
Hoja binafsi ya Mnyika ilikuwa ni kupendekeza Bunge lijadili na kupitisha maazimio ya hatua za haraka za kuboresha upatikanaji wa maji safi na ushughulikiaji wa maji taka katika jiji la Dar es Salaam, hoja ambayo ilitupiliwa mbali na kuzua mtafaruku bungeni.
Hoja nyingine ni ya Mbunge wa Kuteuliwa na Rais, ambaye pia ni mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia aliyoitoa bungeni juu ya udhaifu wa mitaala ya elimu nchini.
 
Pamoja na katazo hilo la polisi kuhusu kutokuwepo kwa maandamano hayo, lakini maandalizi yalipamba moto huku magari yenye vipaza sauti yakiwa yameandaliwa katika ofisi za makao makuu ya Chadema, Kinondoni ili  kuwahamasisha watu kujitokeza kwenye maandamano hayo ya kuwapokea wabunge wao.
 
CHANZO: NIPASHE

Makinda awafinya Sitta, Zitto, Lowassa

Spika wa Bunge Mh. Anna Makinda

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimedhamiria kumtumia Spika wa Bunge, Anne Makinda, kuandaa mkakati wa kuwaumbua na kuwazima kisiasa wanasiasa kadhaa wa CCM na upinzani wanaosemekana kuwa “wasumbufu”, wakiwamo Spika aliyepita Samuel Sitta, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto, na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa.

Katika kutekeleza dhamira hiyo, Makinda anachukua hatua mbalimbali za kiutawala, zenye lengo la kupunguza makali ya wanasiasa hao, wanaoonekana kuwa na malengo mapana ya kisiasa mbele ya safari.
Mbali na hilo, Makinda, ambaye pia anasemekana “kuwekwa mfukoni na serikali” amedhamiria kupunguza nguvu za upinzani kwa ama kutumia kanuni za Bunge au kuvunja baadhi ya kanuni hizo.

Katika kutekeleza moja ya hatua hizo, jana Makinda alifanya mabadiliko makubwa ya kamati za Bunge, akafuta baadhi ya misingi iliyoachwa na Sitta.
Katika kukamilisha mpango huo, Makinda aliunganisha kamati mbili za Bunge zilizokuwa zinaongozwa na wabunge wa upinzani - Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma iliyokuwa chini ya Zitto na Kamati ya Hesabu za Serikali iliyokuwa chini ya John Cheyo wa UDP.

Maana yake ni kwamba, Zitto na Cheyo watalazimika kupigiwa kura ili apatikane mmoja wa kuongoza kamati mpya.
Baadhi ya wachambuzi wa habari za siasa wanasema kimantiki iliyovunjwa ni kamati ya Zitto, ambayo inaunganishwa na ya Cheyo.
Wanasema lengo ni kumaliza nguvu na machachari ya Zitto, ambaye hana ukaribu na CCM kama alivyo Cheyo.

Mbali ya mkakati huo wa kumkomoa Zitto, Makinda pia ana mkakati wa kupunguza idadi ya wapinzani katika Kamati ya Uongozi ya Bunge kutoka watatu hadi wawili.
Wachambuzi wanasema hizi ni jitihada za Makinda kufuta nyayo za Sitta, kwani ndiye aliyepitisha kanuni zilizowapatia wapinzani kamati tatu, na kuingiza wajumbe watatu wa upinzani katika kamati ya uongozi.

Makinda hakuishia hapo. Amevunja pia Kamati ya Ulinzi, Usalama na Mambo ya Nje, ambayo pia iliasisiwa na Sitta.
Lakini tafsiri pana ya uamuzi huo ni kwamba, kwa kuivunja kamati hiyo na kuunda mbili, amemfanya Lowassa aongoze Kamati ya Ulinzi na Usalama, huku ya nje ikitafutiwa mtu mwingine.

Wajuzi wa siasa za ndani ya CCM wanasema uamuzi huo umelenga kumnusuru Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Bernard Membe, ambaye hakuwa anapenda wizara yake kuwekwa chini ya kamati inayoongozwa na Lowassa.
Ikumbukwe Membe amekuwa akitajwa kuwa hasimu wa kisiasa wa Lowassa ndani ya chama katika kinyang’anyiro cha kuwania urais 2015.

Miezi kadhaa iliyopita, Membe alilalamikia hatua ya kamati ya Lowassa kutembelea balozi za Tanzania nje ya nchi, hasa Ulaya na Marekani.
Malalamiko hayo yalihisiwa kwamba kuna jambo Membe hakutaka kamati ya Lowassa ilijue katika balozi zetu; na kwa mantiki hiyo hakutaka kuwajibika kwake kwa sababu za ushindani wao wa kisiasa.

Mbali na Membe, mtu mwingine ambaye amekuwa hasimu wa kisiasa kwa miaka ya karibuni ni Sitta, ambaye aliunda kamati iliyofanya uchunguzi wa sakata la Richmond, ambalo lilimfanya Lowassa ajiuzulu uwaziri mkuu mwaka 2008.
Kwa kuwa na wizara ya Sitta ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki ilikuwa chini ya kamati ya Lowassa, kitendo cha Makinda kuiondoa kwake kinampa ahueni Sitta, ambaye naye asingependa kusimamiwa na kamati inayoongozwa na Lowassa.
Baadhi ya wabunge wanaomkosoa Makinda, pamoja na kutambua kuwa anafanya hivyo kumnusuru Membe na kupalilia sokomoko la kisiasa ndani ya CCM, wamesema analenga pia kudhoofisha nguvu ya upinzani bungeni.

Wanasema anafanya hivyo ili kujipendekeza kwa serikali na CCM, huku akilenga kuwania tena uspika 2015, kipindi ambacho tayari ameshatangaza kuwa hatagombea ubunge.
Miongoni mwa mawaziri ambao wanasemekana kutumiwa na serikali kumdhibiti na kumpotosha Makinda ni William Lukuvi.

Vile vile, wachambuzi wanasema hakuna mantiki ya kuivunja kamati ya Zitto, yenye kushughulikia mashirika 280, halafu ikaunganishwa na kamati yenye majukumu mazito kama ya Cheyo.
Wanadai Makinda anakusudia kupunguza makali ya kamati tatu nyeti zilizokuwa zinatumiwa na wapinzani kuleta uwazi zaidi katika kuisimamia serikali.
Kamati ya wapinzani ambayo haikuguswa ni ya Hesabu za Serikali za Mitaa inayoongozwa na Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema (TLP), anayesemekana kuwa kipenzi cha CCM na Rais Jakaya Kikwete.

Kabla yake, kamati hiyo ilikuwa inaongozwa na aliyekuwa Mbunge wa Karatu, Dk. Willibrod Slaa (CHADEMA).
Kamati hizi zimekuwa msaada mkubwa sana kwa kusimamia fedha za serikali kuu na zile za mitaa, lakini kwa mabadiliko yaliyofanywa na Makinda, wapinzani watabakiwa na fursa finyu.

Kwa siku za karibuni, Zitto ameonekana kuisumbua serikali katika masuala mbalimbali, na alitoa matamko makali katika sakata la gesi ya Mtwara.
Kijumla huu ni mkakati wa Makinda kuidhibiti CHADEMA bungeni ili isiongoze kamati nyeti, kwani hata jinsi Mrema na Cheyo walivyopewa fursa hizo, ilitokana na kupindwa kwa kanuni.

Kimsingi kamati zao zilipaswa kuongozwa na wabunge wa CHADEMA ambao kikanuni ndio wanaunda kambi rasmi ya upinzani bungeni.
Baadhi ya wabunge wanasema huu ni ushahidi mwingine wa ubabe wa Makinda, kwani kanuni za Bunge hazijabadilishwa ili kumwezesha kuunda na kuvunja kamati hizi mpya.


Mitaala yamtesa Waziri Kawambwa

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi Mh. Shukuru Kawambwa
  • MBATIA ATOA KASORO NNE KUPINGA ILE ILIYOLETWA BUNGENI
HOJA binafsi ya mbunge wa kuteuliwa na Rais, James Mbatia, aliyeibana serikali kutaka ilete bungeni nakala ya mitaaala ya elimu nchini, imezidi kumweka pabaya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa. Nakala ya mitaala hiyo ambayo imezua mjadala ndani na nje ya Bunge kwa wiki nzima sasa, ilikabidhiwa kwa wabunge jana na kuibua mzozo mpya.

Mara baada ya Spika Makinda kugawa nakala hizo na kulieleza Bunge kuwa mitaala hiyo ni halali, Mbatia alikuja juu kuomba mwongozo wa Spika kupinga uhalali wake. Mbatia ambaye pia ni mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, aliainisha kasoro nne kuonyesha kwamba mitaala hiyo imechakachuliwa.

  1.  Alisema aliomba kuletewa nakala ya mitaala ya elimu ya kutoka mwaka 1977 hadi 2005, lakini nakala ya mitaala iliyoletwa bungeni ni ya mwaka 1978 hadi 2005.
  2. Pili alisema mitaala iliyoletwa bungeni imechakachuliwa kwani haina ISB namba inayotolewa na Bodi ya Maktaba Nchini.
  3. “Tatu, alisema mitaala hiyo haina saini ya Kamishna wa Elimu Nchini kwani lazima asaini kuonyesha mitaala hiyo ni halali na ni mali ya serikali. “Ukiangalia kwenye muhtasari huu wa elimu nilioushika hapa, kuna ISB namba inayotolewa na Bodi ya Maktaba na imesainiwa na Kamishna wa Elimu. Hii mitaala lazima pia isainiwe na Kamishna wa Elimu na iwe na ISB, lakini hii haina,” alisema Mbatia.
  4. Kubwa kuliko yote, Mbatia alisema mitaala ya elimu inapaswa kuwa ya Tanzania nzima, lakini hii iliyoletwa bungeni imeandikwa kwa ajili ya Tanzania Bara tu, jambo ambalo sio sahihi. Katika mwongozo huo ambao haujatolewa uamuzi, Mbatia aliliomba Bunge lijadili mitaala hiyo kubaini kama ni sahihi.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi huo wa Bunge, alisema serikali imeshindwa kuleta kile alichokitaka hivyo hawezi kujiuzulu.

Naye Waziri Kawambwa alipozungumza na wanahabari nje ya ukumbi wa Bunge, alisema kuna makosa ya uchapaji ndio maana mitaala hiyo imeandikwa kutoka mwaka 1978 hadi 2005 badala ya 1977 hadi 2005.
Kuhusu saini ya Kamishna wa Elimu, alikiri kuwa kweli haina saini yake lakini ameandikia hati kuonyesha uhalali wa mitaala hiyo. Waziri Kawambwa alikiri kuwapo kwa kosa lingine la uchapaji linaloonyesha mitaala hiyo ni kwa ajili ya Tanzania Bara wakati ilipaswa kusomeka kuwa kuwa ni kwa ajili ya Tanzania nzima. Alisema pamoja na kasoro hizo za uchapaji, mitaala hiyo ni halisi na ndiyo inayotumika kwa sasa.

Mmoja wa wajumbe wa tume iliyoundwa kuchunguza uhalali wa mitaala hiyo, Mchungaji Israel Natse, alisema kulikuwa na ubishani mkubwa kwenye kamati kuhusu kasoro hizo. “Kibaya zaidi tulipewa hadidu za rejea moja tu inayosema tuangalie uhalali wa mitaala hiyo. Hivyo hatukuwa na wigo mpana kuchambua kasoro hizo,” alisema.
Awali akikabidhi nakala hizo, Spika wa Bunge Anne Makinda alisema Bunge liliunda kamati ya wabunge sita kuthibitisha mitaala hiyo kama ni halali au la. “Napenda kuwaarifu wabunge kuwa kamati hiyo imemaliza kazi yake na nyaraka hizo ni halali na sasa nazigawa kwenu,” alisema.

Timu hiyo iliundwa juzi na Naibu Spika, Job Ndugai, kupitia nakala hizo ili kubaini kama ni halisi au la kabla ya kukabidhiwa kwa wabunge. Mwenyekiti wa tume hiyo ni Magreth Sitta na wajumbe wake ni Bernadetha Mshashu, Jabir Malombo, Khalifa Khalifa, Mchungaji Israel Natse na Yahya Kassim Issa

Tanzania Daima


Thursday, February 7, 2013

Ujerumani itatetea msimamo wake mjini Brussels

Mkutano muhimu wa kilele kuhusu mustakbal wa Umoja wa Ulaya unalenga kuweka kando masilahi ya kitaifa,na kuafikiana kuhusu bajeti ya kugharimia miradi ya kubuni nafasi zaidi za kazi hadi ifikapo mwaka 2020
"Ulaya yenye nguvu bila ya kulazimika kutoa pesa zaidi":huo ndio msimamo ambao Ujerumani inatapanga kuutetea katika mazungumzo ya kubuni bajeti ya muda mrefu ya Umoja wa Ulaya.Pale viongozi wa taifa na serikali wa mataifa 27 watakapokutana kuanzia leo alkhamisi hadi kesho ijumaa mjini Brussels,serikali kuu ya Ujerumani inataka kuona gharama zote za Umoja wa Ulaya katika kipindi cha mwaka 2014 hadi 2020 zinaambatana ipasavyo na mahitaji halisi.Matumizi bora ndio kauli mbiu ambayo kwa kansela Angela Merkel haimaanishi chengine isipokuwa kupunguzwa bajeti ya Ulaya ya mabilioni ya Euro.
Ujerumani inachangia moja kwa tano ya bajeti jumla ya Umoja wa Ulaya kiwango ambacho kinafikia Euro bilioni 200 ikizingatiwa bajeti ya kuanzia mwaka 2007 hadi mwaka huu wa 2013.Wakati wa mkutano pamoja na waziri mkuu wa Italy Mario Monti hapo awali mjini Berlin,kansela Angela Merkel alikumbusha kwamba"Ujerumani ni mojawapo ya wachangiaji wakubwa miongoni mwa nchi za Umoja wa Ulaya,Na hiyo ndio maana wanapendelea kuona kwamba fedha zinatumiwa kwa namna ambayo zitachangia ipasavyo kuufanya Umoja wa Ulaya uzidishe bidii na kuwa uwanja muhimu wa mashindano ya kibiashara."
Upinzani wa nchi za kusini mwa ulaya
 
Kansela Angela Merkel na waziri mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy mjini Berlin

Hata alipokutana na waziri mkuu wa Hispania Mariano Rajoy na rais Francois Hollande wa Ufaransa,hakuchelea kansela kutilia mkazo madai ya Ujerumani,siku chache kabla ya mkutano huo wa kilele kuanza.
Sambamba na kupunguza nakisi,kanasela Angela Merkel anataka pia matumizi katika bajeti ya pamoja ya Umoja wa Ulaya yawekewe kikomo.
"Matumizi ya Umoja wa Ulaya yanabidi yasiruhusiwe kupindukia asili mia moja ya pato la kijamii katika Umoja wa Ulaya-amesema mchambuzi wa masuala ya fedha wa Umoja wa Ulaya Friedrich Heinemann wa taasisi ya uchunguzi wa kiuchumi ya mjini Mannheim.Inamaanisha kwamba bajeti ya Umoja wa Ulaya iongezeke tu ikiwa shughuli za kiuchumi za nchi za Umoja huo zitanawiri na kwa namna hiyo kuongezeka pia pato la ndani la kila mkaazi wa Umoja wa ulaya.
Nchi nyingi za Umoja wa Ulaya,ikiwa ni pamoja na Austria,Finland,Itali,Uholanzi na Sweden zinauunga msimamo wa Ujerumani.Lakini nchi zinazopokea misaada mfano wa Uhispania,Ureno,Ugiriki na nyengine zinaupinga.
Ajira ya vijana ndio kipa umbele
 
Vijana katika juhudi za kutafuta kazi
 

Ujerumani inataka kuona fedha nyingi zaidi zikitolewa kugharimia miundo mbinu ya nishati na miradi ya uchunguzi barani Ulaya.Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya inapendekeza Euro bilioni 120 kwaajili ya miradi hiyo.Katika bajeti ya mwaka 2007 hadi mwaka huu wa 2017 asili mia 80 ya bajeti ya Umoja wa Ulaya ilikuwa ikitumika kusaidia shughuli za kilimo na miradi mengine ya kimkoa.Ujerumani ingependelea kuona fedha za kughamiria miradi ya kilimo na kimkoa zinafutwa.Katika wakati ambapo Ufaransa inataka kuona fedha hizo zinaendelea kutolewa Ujerumani inataka kuona zinatumika kupambana na ukosefu kazi miongoni mwa vijana.