Wanajeshi wa Mali wampokea msaada kutoka kwa Ufaransa na sasa Uingereza inataka pia kuwasaidia
Serikali ya Uingereza 
inatarajiwa kujadili mpango wa kutoa msaada zaidi kwa wanajeshi wa 
Ufaransa wanaopambana na waasi nchini Mali.
Waziri mkuu David Cameron, amesema kuwa huenda 
msaada za usafiri na kijasusi ukatolewa kwa wanajeshi hao. Ndege mbili 
za kijeshi tayari zimetolewa kwa jeshi la Ufaransa.
Waziri wa ulinzi anasema kuwa hakuna mipango ya kufanya mashambuli ya ardhini kwa sasa.
Kuhusu vifo vya raia wa Uingereza katika 
mashambulizi kwenye kiwanda cha gesi nchini Algeria yaliyofanywa na 
wapiganaji wa kiisilamu, bwana Cameron alisema kuwa eneo la Kaskazini 
mwa Afrika linageuka kuwa ngome ya wapiganaji wa kiisilamu.
Wasiwasi kuhusu athari za kundi la kigaidi la 
al-Qaeda katika ukanda huo, zinaonekana kudhibitiwa kufuatia mpango wa 
kuwapeleka wanajeshi wa Ufaransa kupambana na wapiganai wenye uhusiano 
na Al Qaeeda nchini Mali na Algeria ambako waliwateka nyara wafanyakazi 
wa kigeni.
Wanamgambo waliowashambulia wafanyakazi wa 
kigeni nchini Algeria, ambapo takriban mateka 48 waliuawa wametoa wito 
kwa Ufaransa kusitisha harakati zao nchini Mali.
''magaidi kuhangaishwa''
Waiziri mkuu alisema kuwa Uingereza pamoja na 
washirika wake wako katika mapambano dhidi ya kasumba ambayo inatia doa 
kubwa dini ya kiisilamu na ambayo inaamini kuwa mauaji na ugaidi 
yanakubalika na tena ni sharti yafanyike.
Jibu la jamii ya kimataifa kwa tisho hili liitakuwa swala muhimu katika ajenda ya mkutano wa nchi nane zilizostawi duniani G8.
"lazima tupambane na hao magaidi kwa kutumia 
mbinu zote za kuweka usalama. Lazima tuwakomeshe, kijeshi. Ni lazima 
tuzungumzie hii kasumba yao, sharti tufunge hii nafasi wanayoitumia, 
kuendesha harakati,zao'' alisema waziri mkuu.
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

0 Maoni:
Post a Comment