Tuesday, June 12, 2012

CCT yaitaka serikali kusitisha uchimbaji wa Urani

Dk. Peter Kitula

Serikali imesema masuala ya dini wala kabila hayataingizwa kwenye dodoso la Sensa yawatu na makazi kwa sababu maendeleyo hayapangwi kwa kuzingatia vigezo hivyo.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mkuu , Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dk. Albina Chuwa, kwenye mkutano waviongozi wa dini kuhusu maandalizi ya Sensa ya watu na makazi mwaka 2012 iliofanyika mjini hapa.

“Aidha, ikumbukwe kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ibara namba 19 imetoa uhuru wa kuabudu kwa kila mtu, lakini pamoja naukweli kwama wananchi wa Tanzania wana dini serikali haina dini, msimamo huu umeendelea kuzingatia kwenye sera ya utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya maendeleo na ndiyo maana inasifika kwa amani, utulivu na mshikamano ambao sote tunatakiwa tujivunie na kuuenzi,” alisema.

Alisema kuwa sheria ya takwimu inatamka wazi kuwa NBS ndiyo yenye mamlaka ya kutoa takwimu rasmi hapa nchini.

“Hivi karibuni kumetokea baadhi ya watu au vikundi kuanza kutoa takwimu kupitia mitandao mbalimbali ya idadi ya Wakristo, Waislamu na wapagani, ninaomba kutamka rasmi kuwa takwimu hizo sio rasmi na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haizitambui takwimu hizo kwa vile ofisi ya Taifa ya Takwimu ndiyo yenye mamlaka ya kutoa
takwimu rasmi za serikali,” alisema.





CHANZO: NIPASHE

0 Maoni:

Post a Comment