Monday, January 27, 2014

Edward Snowden won't be pressured to end asylum, Russia says

National Security Agency leaker Edward Snowden poses with German Green party parliamentarian Hans-Christian Stroebele in Moscow on October 31. Stroebele returned from the meeting with a letter from Snowden to German authorities, which was distributed to the media. In it, Snowden said he is confident that with international support, the United States would abandon its efforts to "treat dissent as defection" and "criminalize political...

KATIBU WA CCM MBEYA AKOMBWA NA M4C PAMOJA DAIMA

Aliyekuwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tawi la Isitu, Chimara mkoani Mbeya, Felix Komba jana alizolewa na Operesheni ya M4C Pamoja Daima ya Chadema na kuamua kukikacha chama chake na kujiunga na chama hicho. Operesheni hiyo ya Chadema inayozunguka nchi nzima imeendelea kushika kasi kutokana na maelfu ya wananchi kujitokeza katika mikutano ya chama hicho. Operesheni hiyo imezidi kuwa tishio...

Wednesday, October 23, 2013

Kamati ya Zitto shakani • MAKAMU WAKE ASEMA HAJUI KINACHOENDELEA

Hata hivyo, kamati hiyo imezua mashaka ya vyama hivyo kuhojiwa kwani pamoja na Zitto kutoa taarifa kuwa atakuwa nje ya nchi kikazi, makamu wake, Deo Filikunjombe, naye amedai yuko jimboni na hajui kinachoendelea kuhusu vyama hivyo. Akizungumza na gazeti hili jana kuhusu madai ya vyama hivyo kutopewa taarifa ya wito kwa maandishi, Filikunjombe alisema yuko jimboni kwa wapiga kura wake. “Naomba usubiri niweze kuwasiliana na wajumbe wengine walioko...

Vyama vyakabidhi mapendekezo sheria ya katiba

Hatimaye vyama vya siasa vilivyo na uwakilishi, kikiwamo Chama Cha Mapinduzi (CCM) na visivyokuwa na uwakilishi bungeni vimewasilisha serikalini mapendekezo ya kuboresha sheria ya marekebisho ya Sheri ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2013. Msemaji wa vyama hivyo, ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, aliwaambia waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuwa mapendekezo hayo yalikabidhiwa kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya...

Filikunjombe awachana mawaziri mbele ya JK, Wananchi Mlangali/Mbwila wazuia msafara wa Rais

MBUNGE wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe awafyatua mawaziri mbele ya Rais Jakaya Kikwete kuwa wamekuwa wakitembelea jimbo lake la Ludewa wakati wa ziara ya Rais na waziri mkuu wakati siku zote wananchi wa jimbo hilo wanalia kwa kero mbali mbali. Mbali ya kuwawasha mawaziri hao pia mbunge Filikunjombe amesema kuwa kero ya maji katika mji wa Ludewa ni kubwa na wananchi kwa zaidi ya wiki moja sasa hawana maji yamefungwa kwa ajili ya kuelekea...

Tuesday, October 15, 2013

Raila Odinga aeleza Nyerere alivyomsaidia kusoma nje

Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Odinga ameeleza kuwa bila ya Pasipoti ya Tanzania aliyopewa kwa msaada na Mwalimu Julius Nyerere asingeweza kwenda Ujerumani kusoma baada ya Idara ya Uhamiaji ya Kenya kumnyima hati hiyo ya kusafiria. Odinga ambaye hivi sasa ni kiongozi mkuu wa Muungano wa Cord ameeleza hayo katika kitabu chake kiitwacho The Flame of Freedom, ambamo ameelezea historia yake na familia yake katika mambo mbalimbali. Idara...

Je ICC inaonea Afrika?

Huku Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akikabiliwa na shinikizo kufika mbele ya mahakama ya kimataifa ya jinai ICC mwezi ujao, kujibu mashitaka ya uhalifu dhidi ya binadamu dhidi yake , Muungano wa Afrika umeitisha mkutano maalum kujadili uhusiano wake na mahakama ya ICC. Muungano wa Afrika wenyewe umekumbwa na mgawanyiko kuhusu mahakama ya ICC, huku viongozi wa Afrika Mashariki wakikabiliwa na upinzani kutoka kwa wenzao wa Afrika Magharibi wanaounga...

Thursday, October 10, 2013

Ziara ya Zitto Kabwe kanda ya Magharibi,jimbo la Igalula

Siku ya 5 ya ziara ya CHADEMA Kanda ya Magharibi imetufikisha Jimbo la Igalula, wilaya ya Uyui. Tumekutana na wananchi katika vijiji vya Goweko, Loya, Miswaki, Miyenze na Kigwa. Tumezungumza kuhusu changamoto ya usafiri wa Reli, wafugaji kunyanyaswa na watendaji wa kata na askari kwa kunyanganywa mifugo, zao la Tumbaku, maji safi na salama na suala la jumla la Katiba na mchakato wa kuandika katiba. Kimsingi shughuli za kiuchumi...

Dk. Slaa aibamiza CCM

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema kuwa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imekuwa janga la Watanzania. Amefafanua kuwa CCM inaua ubunifu wa vijana, kwamba asilimia 90 ya wanafunzi wanafeli shuleni huku viongozi wa chama hicho wakiwahadaa wananchi kwamba wanaleta maendeleo. Dk. Slaa alitoa kauli hiyo jana alipozuru Shirika la Anga la Marekani (NASA) huko Huntsville nchini Marekani,...